HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma imefanikiwa kutoa chanjo ya surua-rubella kwa Watoto 32,272 wenye umri wa kuanzia miezi tisa hadi 59.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Kapenjama Ndile amesema idadi hiyo ya Watoto waliopata chanjo ni sawa na asilimia 112 ya lengo la kutoa chanjo kwa Watoto 28,794.
“Mafanikio haya yametokana na uhamasishaji wa jamii kupitia vyombo vya Habari,matangazo kwa njia ya gari la matangazo (PA),mikutano ya hadhara na uhamasishaji uliofanywa na wahudumu wa Afya ngazi ya jamii’’,alisema Ndile.
Wizara ya Afya na Wizara ya Ofisi ya Rais TAMISEMI inaendesha kampeni ya kitaifa ya kutoa chanjo ya surua-rubella kwa Watoto wote wenye umri wa miezi tisa hadi 59.
Mkoa wa Ruvuma umepanga kuchanja chanjo ya surua-rubella kwa Watoto zaidi ya 200,000
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.