• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MASHINDANO ya UMISSETA Ruvuma yalivyoibua vipaji kitaifa na Afrika

Imewekwa kuanzia tarehe: May 29th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed  ameyafungua rasmi mashindano ya michezo ya UMITASHUMTA na UMISSETA mwaka 2024 kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Akizungumza kabla ya kufungua mashindano hayo  ambayo yanashirikisha Halmashauri zote nane,Mkuu wa Mkoa amesema ubora wa wachezaji katika timu nyingi hasa mchezo wa soka wameanzia mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA hatimaye kuchukuliwa na vilabu vikubwa.

Ametolea mfano mashindano ya UMISSETA katika Mkoa wa Ruvuma yamewatengeneza vijana kupitia timu ya soka iliyoshiriki mashindano hayo katika ngazi ya Taifa na Mkoa kuibuka mshindi wa kwanza hivyo kuchukua kikombe cha UMISSETA Taifa mwaka 2019.

“Baadhi ya vijana kutoka Ruvuma hawakuishia hapa,walishiriki mashindano hayo katika ngazi ya Afrika Mashariki,ushiriki wao katika ngazi hizo ulifanya wachezaji kama Nathaniel Chilambo anayechezea timu ya Azam Sports  kuibuliwa,Golikipa wa Timu yetu ya UMISSETA Mkoa Nice Kahemela ambaye kwa sasa anachezea Sports Academy iliyopo nchini Afrika ya Kusini ’’,alisema Kanali Abbas.

Mkuu wa Mkoa amewataja wachezaji wengine walioibuliwa kutokana na mashindano ya UMISSETA Ruvuma kuwa ni Neva Kabona kwa sasa yupo Zanzibar anachezea timu ya JKU,kijana mwingine ni Simba Simba ambaye baada ya mashindano hayo alipata ufadhili wa Kwenda kusoma nchini Marekani na John Chikungu ambaye hivi sasa ni mchezaji wa Ruvuma Shooting.

“Nimeona niwataje wachezaji hawa ili mjue kuwa mashindano haya yakitiliwa msukumo unaostahili ni faida kubwa kwa vijana wetu na Taifa letu’’,alisema Mkuu wa Mkoa.

Amebainisha Zaidi kuwa serikali kwa kutambua umuhimu wa michezo,Sanaa na utamaduni imeongeza tasnia ambazo zitakuwa chachu kwa vijana ili kuinua vipaji katika mitaala ya elimu.

Hata hivyo amesisitiza kuwa malengo ya kuinua vipaji vya vijana yatafikiwa iwapo wadau wote wanaohusika na michezo watashirikiana na kufanya kazi kwa Pamoja ambapo amesema serikali imeanza kuimarisha michezo kwa kutenga shule 56 kati ya hizo shule tatu zipo mkoani Ruvuma ambazo ni Songea Boys,Maposeni na Mahanje.

Awali akitoa taarifa ya mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA ,Kaimu Afisa Elimu wa Mkoa wa Ruvuma Mathias Tilia  amesema katika mashindano ya mwaka huu jumla ya wanafunzi 658  wanashiriki mashindano ya Mkoa mwaka huu ili kupata wanafunzi  120 ambao watawakilisha Mkoa  wa Ruvuma kwenye mashindano ya kitaifa yanayofanyika mkoani Tabora.

Kaulimbiu ya Michezo ya UMITASHUMTA na UMISSETA mwaka huu inasema Tunajivunia mafanikio katika sekta ya elimu,michezo na Sanaa,hima Mtanzania shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa 2024.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.