• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MATAMASHA yatumike kukemea vitendo vinavyokiuka mila na desturi za Mtanzania

Imewekwa kuanzia tarehe: February 26th, 2023

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Makumbusho ya Taifa Tanzania Dkt. Oswald Masebo  ameshauri matamasha ya kumbukizi yatumike kukemea vitendo viovu vinavyokwenda kinyume na mila na desturi ya mtanzania.

Dkt.Masebo ametoa ushauri huo kwenye kongamano la kumbukizi ya mashujaa wa vita ya Majimaji lililofanyika kwenye ukumbi wa Crasta mjini Tunduru.

Kongamano hilo ni sehemu ya kumbukizi ya miaka 117 ya mashujaa wa vita ya Majimaji waliuawa na wajerumani Februari 27,1906 kwa kunyongwa mashujaa 67 na wajeruamni katika eneo la Songea Klabu na kuzikwa ndani ya makumbusho yaTaifa ya Majimaji Mahenge Songea.

Mwenyekiti huyo wa Bodi ya Wakurugenzi wa Makumbusho  amesema,hivi sasa Taifa lipo katika vita ya kupambana na watu wanaoharibu mila na desturi za mtanzania ambapo kumekuwa na mmomonyoko wa maadili kwa Watoto na vijana.

“Hivi sasa vitendo vya kishoga ambavyo ni kinyume na mila na desturi zetu vimekuwa tishio kubwa kwa vijana wetu,hivyo tunapofanya kumbukizi kama hii ya mashujaa wa vita ya Majimaji inatakiwa sote kukemea kwa nguvu zote ili kulinusuru Taifa kuingia kwenye janga kubwa la mmomonyoko wa maadili’’,alisisitiza Dkt.Masebo 

Akizungumza wakati wa ufungaji kongamano hilo ambalo lilishirikisha wadau mbalimbali kutoka mkoa wa Ruvuma ,Wizara ya Maliasili na Utalii na watoa mada kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam,mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe.Ngollo Malenya ameipongeza Wizara kwa kufanya kongamano hilo kwa mara ya kwanza katika wilaya ya Tunduru.

Mheshimiwa Malenya ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo amesema wilaya ya Tunduru  ndiyo kiini cha ukombozi wa nchi ya Msumbiji kwa kuwa mipango yote ya harakati za ukombozi wa nchi hiyo zilifanyika katika Kijiji cha Masonya Tunduru ambapo hayati Baba wa Taifa Mwl.Julius Nyerere na Hayati Samora Michel wa Msumbiji  walipanga mipango yote hadi nchi ya Msumbiji ilipopata uhuru wake mwaka 1975.

Mkuu wa Wilaya ametoa rai kwa vijana walioshiriki kwenye kongamano hilo kuacha mila na desturi za kigeni badala yake kufuata maelekezo ya wazee kwa kuzingatia maadili,mila na desturi ili kulinda utamaduni wa mtanzania.

Katika kongamano hilo  mapendekezo mbalimbali yalitolewa ikiwemo mapendezo ya kurejeshwa hapa nchini malikale zote za Mkoa wa Ruvuma zilizopo nje ya nchi na wanafunzi katika shule za sekondari na vyuo kila mwaka kuhakikisha wanashiriki  kikamilifu kwenye matamasha ya mil ana utamaduni ili kurithisha historia ya Tanzania.

Mada mbalimbali ziliwasilishwa zikiwemo kutoka kwa wahadhari wa chuo kikuu cha Dar es salaam na Wataalam wa Makumbusho ya Taifa zikiwemo nafasi ya ndumba katika vita,urithi na utamaduni wa wangoni na utamu wa historia ya Mkoa wa Ruvuma.

Kilele cha miaka 117 ya kumbukizi ya mashujaa  67 wa vita ya Majimaji kinatarajiwa kufanyika Februari 27,2023 katika Makumbusho ya Taifa ya Majimaji mjini Songea ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.

Imeandikwa na Albano Midelo wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mkoa wa Ruvuma

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.