Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma imedhamiria kuondokana kabisa na utegemezi kutoka Serikali Kuu linapokuja suala la utekelezaji wa bajeti yake ifikapo mwaka 2050.
Dhamira hiyo imetolewa kwenye mkutano uliowaleta pamoja wadau mbalimbali kutoa maoni kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025-2050.
Kwa mwaka huu wa fedha (2024/25) mchango wa mapato ya ndani ya Halmashauri ya Mji wa Mbinga ni asilimia 10.4 tu ya bajeti nzima ya Shilingi bilioni 31.6 huku bajeti hiyo ikiitegemea Serikali kuu kwa asilimia 89.6.
Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mapato ya ndani yanachangia asilimia 17.5 ya bajeti nzima ya Shilingi bilioni 48.1 .
Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Kisare Makori amesema kuwa ufanisi katika ukusanyaji mapato ya ndani kwa Halmashauri za Mji wa Mbinga na Wilaya ya Mbinga utachochea utoaji huduma bora kwa wananchi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.