Halmashauri ya Mji wa Mbinga mkoani Ruvuma inatarajia kupata Jumla ya shilingi milioni 845.8 kutokana na mauzo ya viwanja vilivyopimwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo,Grace Quntine amesema kati ya fedha hizo hivyo shilingi milioni 139.6 ni gharama ya umilikishaji ambazo zitaingia serikali kuu na kiasi cha shilingi milioni 719.7 zitaingia Halmashuri ya Mji kutokana ma mauzo ya Viwanja pamoja na ada ya maombi ya kumiliki ardhi.
“Nawakaribisha Wananchi wote wilayani Mbinga,Mkoa wa Ruvuma na watanzania kwa ujumla,Wawekezaji,kampuni pamoja na Taasisi mbalimbali kujipatia viwanja katika wilaya ya Mbinga’’alisema.
Hata hivyo amesema katika kuweka utaratibu wa upatikanaji wa viwanja hivyo mwombaji asiwe na kiwanja au viwanja amabavyo avijaendelezwa ambapo amesisitiza makundi maalum yatapewa kipaumbele.
Amesisitiza kuwa Mwombaji pia atalazimikuka kununua fomu namba 19 yenye gharama fedha za kitanzania shilingi 20,000/=, sambamba na uwezo wa kulipa kiwanja ndani ya siku thelathini.
Amesema Umiliki wa asili pia utapewa kipaumbele katika utaratibu wa utoaji viwanja katika maeneo hayo.
Mkurugenzi huyo amesema kasi ya ukuaji wa Mji wa Mbinga imekua kwa sasa hiyo wataalamu wa Ardhi na mipango Miji katika Halmashauri hiyo wanashauri mwombaji kuendeleza viwanja hivyo ndani ya miezi 36 yaani miaka mitatu.
Mpaka sasa Halmashuri ya Mji wa Mbinga ina Viwanja Zaidi ya 500 ambavyo vinauzwa kwa fedha ya kitanzania Shilingi 1700 kwa mita za mraba ambavyo ni viwanja vya makazi pekee.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.