Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma wameungana na wanafunzi na walimu wa shule ya Msingi Juhudi iliyopo Kata ya Kigonsera kuadhimisha miaka 60 ya Muungano kwa kufanya usafi wa mazingira na kushiriki zoezi la upandaji wa miti.
Shughuli hizo ambazo zimelenga utunzaji na uhifadhi wa mazingira zimefanyika kwenye maeneo mbalimbali ya shule ya msingi Juhudi.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wakati wa zoezi hilo, Bw. Pascal Ndunguru ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ametoa wito kwa jamii kuwa na utamaduni wa kutunza mazingira pamoja na kuendelea kupanda miti katika maeneo yao.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.