AFISA Misitu wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga mkoani Ruvuma Bw. Sota Ndunguru amesema tayari Halmashauri hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa misitu, imezalisha miche milioni 1.6 ili kuendeleza kampeni ikiyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ya kupanda miti milioni 4.9 hadi kufikia Aprili 2024.
Ndunguru amesema hayo wakati anazungumza kwenye kampeni ya upandaji miti uliofanyika katika shule ya Msingi Mkwaya, Kata ya Kilimani wilayani humo.
“ Katika mwaka wa fedha 2023/24 Halmashauri ya Mji wa Mbinga kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa misitu imezalisha miche ya miti milioni 1.6 tumevuka lengo kwa asilimia 6.7 “,alisema Bw. Ndunguru.
Ameitaja miche ya miti iliyozalishwa ni ya matunda, rafiki ya maji,, miti ya mbao,kivuli na mapambo.
Amebainisha kuwa kari ya miche ya miche ya kivuli, mbao na mapambo ni milioni 1.347, matunda 232, 890 na na miche rafiki kwenye vyanzo vya maji 22, 920.
Wakizungumza kwenye kampeni hiyo baadhi ya madiwani wamewaagiza walimu wakuu kuweka utaratibu wa kila mwanafunzi kupanda mti na kuumiliki mti wake na kuhakikisha anautunza.
Madiwani hao pia wamewashauri viongozi wa vijiji kutunga sheria ndogondogo ili kuhakikisha miti inatunzwa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.