KAIMU Mkuu wa Idara ya Viwanda, Bishara na Uwekezaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Bi. Martina Ernest Ngahi ametoa wito kwa wawekezaji waliopo ndani na nje ya Mkoa wa Ruvuma kuja kuwekeza katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Amesisitiza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ina maeneo na fursa nyingi za kichumi hivyo ambazo zinaweza kutumika katika kuleta maendeleo nchini.
Bi. Martina ametoa wito huo wakati akizungumza katika kipindi cha radio MBINGA YETU kinachorushwa na Radio Hekima iliyopo katika Wilaya ya Mbinga.
" Katika Halmashauri yetu tuna fursa mbalimbali za kiuchumi mfano uwekezaji wa usindikaji wa sembe au zao la soya, ujenzi wa mahoteli na nyumba za kulala wageni na kadhalika" Amesema Bi. Martina
Kipindi cha MBINGA YETU kinarushwa kila jumamosi kuanzia saa sita mchana hadi saa saba, katika kipindi hiko utapata taarifa mbalimbali za utekelezaji wa shughuli za Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Aidha Bi. Martina amewakumbusha wafanya biashara waliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kuwa wabunifu na kutumia changamoto zilizopo kama fursa katika kuanzisha au kuimarisha biashara zao.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.