HALMASHAURI ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma imevuka lengo katika ukusanyaji wa mapato kwa kukusanya mapato ya ndani kiasi cha shilingi Bil. 6.478 katika mwaka wa fedha 2022/ 2023 ulioanza Julai 01, 2022 hadi Juni 30, 2023.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo mheshimiwa Deusderius Haule amesema Makisio ya awali ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2022/2023 yalikuwa Shilingi 4,598,598,800 yakijumuisha mapato lindwa na mapato halisi.
Amebainisha kuwa Mapato hayo yametokana na kodi na tozo, miamala ya kibiashara,tozo na ushuru mbalimbali,misaada kutoka nje pamoja na mapato mengineyo.
Haule ameyataja kuwa jumla ya mapato ya Ruzuku yaliyopokelewa ni Shilingi Bil. 30.7 fedha ambazo zimetumika kwa matumizi ya kawaida na maendeleo kama vile stahiki za watumishi, manunuzi ya huduma mbalimbali,matengenezo pamoja na haki za kijamii.
Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya usimamizi wa Menejimenti,Ufatiliaji na Ukaguzi (MMI) Mkoa wa Ruvuma Phiniel Mbula ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kwa kusimamia ukusanyaji wa mapato ameitaka Halmashauri hiyo kuendelea kuimarisha usimamizi katika ukusanyaji na matumizi ya mapato.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.