• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MBUNGE atoa msaada wa vifaa katika hospitali ya Tunduru

Imewekwa kuanzia tarehe: March 1st, 2023

MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma(CCM) Mheshimiwa Mariam Nyoka,ametoa msaada wa vifaa tiba mbalimbali katika Hospitali ya wilaya Tunduru mkoani humo ikiwa ni  kutimiza azima yake ya kupunguza baadhi ya changamoto zilizopo katika Hospitali hiyo na kusaidia upatikanaji wa huduma bora za afya.

Vifaa vilivyotolewa ni mashuka 30  na chandarua 15 kwa  ajili ya wodi ya akina mama,mashine za kupimia  magonjwa yasioambukiza(BP na Sukari) kwa wananchi watakaofika kupata huduma ya matibabu katika Hospitali hiyo.

Akizungumza  baada ya kukabidhi vifaa hivyo Nyoka alisema, msaada huo unatokana na dhamira yake ya muda mrefu kabla hajawa Mbunge  kwa kutoa kile alichonacho kuisaidia jamii yenye shida na kuunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali kuhakikisha nchi yetu inakuwa na watu wenye afya bora.

Alisema,kipaumbele chake cha kwanza  kama Mbunge wa vitu maalum ni  kusaidia katika sekta ya afya kwa kuwa sekta hiyo ni moja ya nguzo kuu  na yenye mchango mkubwa katika kuleta mabadiliko ili kuwa na watu wenye afya njema, wenye uwezo wa kufanya kazi za kujiletea  maendeleo yao na kushiriki kukuza uchumi wa mkoa wa Ruvuma nchi yetu.

Nyoka,amewakumbusha watoa huduma  katika Hospitali hiyo na sekta  yote ya afya mkoani Ruvuma,kutoa huduma bora kwa wananchi bila kubagua kwani ni sehemu muhimu na wajibu wao.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi  wa hospitali hiyo Dkt Athuman Mkonohumo, amemshukuru Mbunge huyo kwa  kutoa vifaa tiba ambavyo vitakwenda kuboresha huduma za afya na kuongeza juhudi za serikali za kuboresha huduma za afya katika Hospitali hiyo.

Dkt Athuman alisema,vifaa hivyo vitawasaidia watumishi kutekeleza vyema majukumu yao ya kila siku na wananchi kupata  huduma bora  za matibabu.

Pia,ametoa wito kwa mashirika,taasisi ,wadau na viongozi wengine wenye uwezo,kujitokeza na kuisaidia Hospitali kwani bado inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwamo upungufu wa vitanda na vifaa vingine kwa ajili ya kuboresha utoaji huduma za afya.

Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali hiyo Nelly Simon amesema,vifaa hivyo vinakwenda kusaidia na kuboresha suala zima la matibabu katika Hospitali hiyo ambayo inakabiliwa na idadi kubwa ya wagonjwa.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.