MBUNGE wa Jimbo la Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma Dkt.Joseph Mhagama amekabidhi Magari mawili ya kubeba wagonjwa katika vituo vya afya Mtyangimbole na Matetereka.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo Dkt.Mahagama amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta magari mapya mawili Katika Jimbo katika Jimbo lake hivyo kurahisisha huduma ya afya kwa wananchi.
“Serikali imetoa fedha za kujenga vituo viwili vya afya na sasa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ametuletea magari mawili ya wagonjwa tunamshukuru sana”,alisema.
Hata hivyo Mbunge huyo wa Madaba amemtaka Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Mtyangimbole kulitunza gari hilo ili liweze kudumu kwa muda mrefu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.