• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MBUNGE Ruvuma ahimiza vijana Tunduru kutumia fursa za kiuchumi

Imewekwa kuanzia tarehe: March 8th, 2023

VIJANA wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma,wametakiwa kuacha tabia ya kulalamika badala yake wazitumie fursa za kiuchumi zilizopo kwa wingi katika maeneo yao kubuni miradi na kufanya kazi kwa bidii na kujiletea maendeleo yao ili kuepuka tabia kuomba omba.

Kauli hiyo imetolewa  na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Ruvuma Mariam Nyoka,wakati akizungumza na baadhi ya vijana wa kijiji cha Wenje kata ya Nalas akiwa katika ziara yake ya kukagua na kuhimiza shughuli mbalimbali za serikali wilayani humo.

Alisema,ili mtu aweze kufanikiwa kimaisha haitaji zaidi ya elimu ya darasani bali ni muhusika mwenyewe kujiongeza kufanya kazi kwa kujituma kwa kila jambo ambalo anatamani kulifikiria na kulifanya.

Nyoka alisema,tatizo la vijana wengi katika wilaya ya Tunduru kukabiriwa na  changamoto ya ukosefu wa ajira na umaskini linatokana na wengi wao kushindwa kubaini na kuzitumia fursa zilizopo katika maeneo wanayoishi na hivyo kuishia kulalamika na kuilaumu serikali yao.

Alisema,hali hiyo inatokana na jamii kukosa moyo wa uthubutu kuingia katika  kazi halali za kuwapatia kipato na kujikuta wakitumia muda mwingi kukaa vijiwemi na kusubiri serikali iwatafutie ajira,jambo ambalo limechangia vijana wengi kuendelea kuwa maskini.

Amewashauri vijana wilayani Tunduru,kuungana ili kupata mikopo isiyo na riba kutoka serikalini na kuwa chanzo cha mapinduzi ya kiuchumi na kuacha kufanya kazi bila malengo na kusisitiza kuwa,vijana wana mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi yetu.

Ametoa wito kwa vijana wa kijiji hicho ambacho kinapakana na nchi jirani ya Msumbuji,kuendelea kulinda na kutunza amani iliyopo na kuepuka kutumiwa kuvuruga mashikamano na utulivu uliopo kwa muda mrefu na kutoa taarifa pindi wanapobaini kuwepo mtu wanayemtilia shaka katika maeneo yao.

Katika hatua nyingine Nyoka,amewataka viongozi wa ngazi mbalimbali, kuhamasisha wananchi wao kuitumia miundombinu inayojengwa na serikali katika maeneo mbalimbali zikiwemo barabara kwa ajili ya kujiletea maendeleo.

Ameipongeza serikali ya awamu ya sita kupitia wakala wa barabara za vijijini na mijini Tanzania(Tarura)mkoa wa Ruvuma kwa kazi nzuri inayofanya ya matengenezo ya barabara ambazo zimewezesha kupitika majira yote ya mwaka na kutoa fursa kwa wananchi wa mkoa wa Ruvuma kufanya shughuli za kujiletea maendeleo.


Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.