WAKULIMA wa zao la mbaazi Mkoani Ruvuma wanufaika kwa kuuza zao hilo kupitia mfumo wastakabadhi ghalani
Hayo yameelezwa na Mrajisi wa mkoa, Peja Mhoja kupitia taarifa mnada wa kwanza zao la mbaazi uliofanyika agosti 30,2022, ambapo bei ilikuwa nzuri kwa wakulima kwani kilo moja imeuzwa kwa wastani wa shilingi 887.00
Alisema wakulima wamepata bei nzuri ya mazao hususani mazao yanayouzwa kupitia mfumo wa stakabadhi za Ghala pia kuwepo kwa ushirikiano nzuri kwa wadau wa stakabadhi ghalani kwa ngazi zote inapelekea mfumo kufanya kazi vizuri.
"Kuwepo kwa matumizi sahihi ya vipimo vya mizani, ambapo inamsaidia mkulima asinyonywe pindi mkulima anapoleta mazoa yake kwenye mfumo, pia kuongezeka kwa uamasishaji wa vyama vya Msingi sinzia navyo vinafanya kazi vizuri na kupelekea kuongezeaka kwa uzalishaji wa mazoa yanauzwa kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani" alisema Mhoja.
Hata hivyo kupitia taarifa hiyo amewasisitiza wakulima ambao wanaouza mazao yao kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani kuongeza uzalishaji wa mazao vile vile watumie mfumo ili waweze kufaidi vyema juhudi zao
Pia katika Mnada huo jumla ya kilo milioni 1.5 za mbaazi ziliuzwa ambapo bei ya wastani ilikuwa shilingi 887.00 nakufanya nakufanya jumla ya malipo kuwa shilingi bilioni 1.3
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.