WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mh Jenista Joakim Mhagama amewataka walengwa wote wanaopokea ruzuku kutoka TASAF wapewe elimu mara kwa mara namna ya matumizi bora ya ruzuku hizo.
Ameyasema hayo jana katika uwanja wa soko la Peramiho A wakati akizungumza na wanufaika wa Mradi huo.
Amesema mpango huu unahakikisha hakuna Mtanzania atakayeachwa nyuma katika utekelezaji wa mapambano dhidi ya kunusuru kaya maskini kwa wananchi.
"Ninaomba Mratibu wa TASAF wa Halmashauri yetu awahamasishe hawa walengwa wa TASAF waanzishe vikundi na kama vikundi vipo mikopo itolewe bila riba ili waweze kujikwamua vizuri kiuchumi", amesisitiza Mh Jenista.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mwalimu Neema Magembe amemuomba Waziri aridhie na kuruhusu Viongozi Ofisi ya TASAF makao makuu Dodoma wafike kutoa Elimu na tafsiri sahihi za miongozo ya utekelezaji wa Mradi huu.
Pia ameongeza kuwa Viongozi hao kutoka makao makuu Dodoma waweze kuwajengea uelewa viongozi wote wa ngazi ya Halmashauri, Tarafa, Kata, Vijiji, Wanakamati na Wananchi wote wanaosimamia utekelezaji wa Mradi wa TASAF kabla ya kuanza kutumia fedha hizo.
Halmashauri ya Wilaya ya Songea ni kati ya Halmashauri nane za Mkoa wa Ruvuma zinazotekeleza Mradi wa mpango wa kunusuru kaya maskini kupitia mfuko wa maendeleo ya Jamii TASAF ikiwa na vijiji 56 na walengwa wanaonufaika ni wanakijiji 6143.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.