Na Albano Midelo
Katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, sekta ya elimu mkoani Ruvuma imepata maendeleo makubwa kupitia miradi mbalimbali ya kimkakati.
Afisa Elimu wa Mkoa wa Ruvuma Mwl. Edith Mpinzile anasema Uwekezaji huu umeleta maboresho makubwa katika miundombinu ya elimu na kuongeza fursa kwa wanafunzi wengi kupata elimu bora.
Ongezeko la Taasisi za Elimu
Mkoa wa Ruvuma umeweza kuongeza idadi ya shule kutoka 841 mwaka 2021 hadi 860 ifikapo 2025 kwa shule za msingi, ikiwa ni ongezeko la asilimia 2.3. Kwa shule za sekondari, ongezeko lilikuwa kubwa zaidi, kutoka shule 214 hadi 247, sawa na asilimia 13.3.
Mkoa wa Ruvuma una vyuo vya maendeleo ya wananchi tisa, vyuo vya ufundi stadi (VETA) vitano, vyuo vya ualimu vitatu, na matawi ya vyuo vikuu matatu.
Fedha na Utekelezaji wa Miradi
Katika kipindi cha miaka minne (2021/2022 – 2024/2025), mkoa ulipokea jumla ya shilingi bilioni 187.07 kwa ajili ya uboreshaji wa elimu. Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 50.15 zilitumika katika mpango wa elimu bila ada, huku bilioni 136.9 zikielekezwa kwenye ujenzi wa miundombinu ya kujifunzia na kufundishia.
Miradi iliyotekelezwa katika kipindi hiki cha uongozi wa Rais Dkt.Samia Sluhu Hassan ni pamoja na Ujenzi wa madarasa 1,717,Maabara 98,Shule mpya 53,Matundu ya vyoo 3,269,Mabweni 102,Nyumba za walimu 106,Vituo vya walimu 13,Ukarabati wa shule kongwe mbili,Mifumo ya maji na uzio kwa shule maalum.
Uboreshaji wa Shule za Sekondari Katika ngazi ya sekondari, miradi kadhaa imekamilika, ikiwa ni pamoja na,Ujenzi wa shule mpya 33 za sekondari za kata,Ujenzi wa shule moja mpya ya wasichana,Ujenzi wa madarasa 1,054,Ujenzi wa mabweni 95,Matundu ya vyoo 878 na Maabara 54.
Sekta ya elimu Mkoa wa Ruvuma pia ilipata magari nane kwa ajili ya shughuli za usimamizi wa elimu na vituo 13 vya walimu viliimarishwa.
Utekelezaji wa miradi ya elimu mkoani Ruvuma umekuwa wa mafanikio makubwa kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Uboreshaji wa miundombinu na utekelezaji wa sera ya elimu bila malipo umesaidia kuongeza fursa kwa watoto wengi zaidi kupata elimu bora.
Haya ni maendeleo yanayodhihirisha dhamira ya serikali katika kuwekeza kwenye kizazi cha baadaye kwa kuhakikisha mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia
.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.