• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MIKAKATI ya kutokomeza kifua kikuu Tunduru,watu zaidi ya 1000 wagundulika

Imewekwa kuanzia tarehe: January 25th, 2023

HOSPITALI ya wilaya Tunduru  mkoani Ruvuma,kupitia kitengo cha kifua kikuu na ukoma imefanikiwa kuibua jumla ya wagonjwa 1,028 sawa na asilimia 122.2 kati ya lengo la kuibua wagonjwa 841  hadi kufikia mwezi Disemba mwaka 2022.

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa wilaya hiyo Dkt Wilfred Rwechugura,wakati akitoa taarifa ya kampeni dhidi ya mapambano ya ugonjwa wa kifua kikuu inayofanyika katika vijiji mbalimbali wilayani humo kwa mwaka 2023.

Dkt Rwechungura alisema,kati ya hao wagonjwa 70 sawa na asilimia 6.8 walikutwa na maambukizi ya VVU    ambapo watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na tano waliokutwa na vimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu  ni 245 sawa na asilimia 23.8.

Kwa mujibu wa Dkt Rwechungura,watoto chini ya miaka mitano wanaoishi na wagonjwa wa kifua kikuu  waliochunguzwa na kupimwa 196 na walioanza dawa kinga185,wanaoishi na wagonjwa wa TB na wakabainika kupatwa na ugonjwa huo ni 17 na waliofariki dunia 17 sawa na asilimia 1.6.

“kimsingi  ugonjwa wa kifua kikuu katika wilaya yetu bado ni tatizo kubwa,hata hivyo tunaendelea na mapambano kupitia kampeni  zinazofanyika katika maeneo mbalimbali,lengo letu ni kutokemeza  kabisa ugonjwa huo”alisema.

Alisema,tatizo la ugonjwa wa kifua kikuu katika wilaya hiyo  linatokana na uwepo wa machimbo ya madini ambayo yana mkusanyiko wa watu wengi, hivyo ni rahisi kuambukizana pamoja na ukosefu wa nyumba bora hasa maeneo ya vijijin.

Dkt Rwechungura, ameitaka jamii kujenga nyumba bora zenye uwezo wa kuingiza hewa ya kutosha na wale watakaona dalili za ugonjwa huo ni vyema kuwahi katika vituo vya kutolea huduma kwa ajili ya uchunguzi badala ya kukaa nyumbani  au kukimbilia kwa waganga wa tiba asili.

Alieleza kuwa,katika kipindi hicho  watu waliogundulika na ugonjwa wa ukoma ni 85 waliopima VVU ni 85 sawa na asilimia 100  na hakuna aliyebainika kupata virusi vya ukimwi.

Aidha alisema, katika kipindi hicho watu wanaoishi na wagonjwa wa Ukoma na wakachunguzwa walikuwa 52,ambapo hakuna aliyegundulika kuwa na ugonjwa huo na wagonjwa wa ukoma  waliopata viatu ni 29 na wagonjwa 37 wana ulemavu wa kudumu.

Amewashukuru wadau wanaotoa huduma za afua mbalimbali za afya zikiwamo za kifua kikuu,ukimwi na ukoma ambao wamekuwa washiriki wazuri katika kuhakikisha afya za wananchi wa wilaya hiyo zinaimarika.

Kwa upande wake Mratibu wa kifua kikuu na ukoma wa wilaya hiyo Dkt Mkasange Kihongole alisema,kwa mwaka 2023 serikali kupitia wizara ya afya imewapa malengo ya kuibua wagonjwa 874.

Alisema,Halmashauri ya wilaya Tunduru kwa kushirikiana na Wizara ya Afya kupitia mkakati wa kudhibiti kifua kikuu na ukoma itahakikisha dawa za kutibu kifua kikuu zinapatikana wakati wote na zinatolewa bila malipo na kuimarisha uwezo wa vituo vya ugunduzi wa TB.

Alitaja mikakati itakayofanikisha kuwapata wagonjwa hao ni kuendelea kutoa elimu  kwa jamii kuhusu ugonjwa huo unavyoenea,dalili na namna ya kujikinga  na maeneo yatakayohusika ni shule za msingi na sekondari za kutwa na bweni.

Mkasange alitaja mkakati mwingine ni kuhakikisha familia zote zinazoishi na wagonjwa wa TB zinafanyiwa uchunguzi na wale watakaobainika wataanzishiwa matibabu  yanayotolewa bila malipo(bure)kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za matibabu.

Alisema, katika kampeni  hizo watashirikiana na wahudumu wa afya ngazi ya jamii  wanaofanya kazi ya kusanya sampuli za makohozi na kuzipeleka Hospitali kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi kwa kutumia mashine za kupimia sampuli za makohozi yaani Gene-Xpert.

Amewataja wadau wengine watakaoshirikiana nao kwenye mapambano ya kifua kikuu ni pamoja na shirika lisilo la Kiserikali la MDH na vyombo vya Habari ambavyo vina mchango na nafasi kubwa ya kupeleka elimu ya ugonjwa huo kwa jamii.

Dkt Mkasange,amewaonya waganga wa tiba asili na tiba mbadala,kuacha tabia ya kuwakumbatia wateja wenye dalili za kifua kikuu ili kuepuka uwezekano wa kuambukizwa wao wenyewe na wateja wanaofika kwenye vilinge vyao.

Mkazi wa mtaa wa Nakayaya Yusufu Juma anayeugua ugonjwa wa kifua kikuu,amewashukuru wataalam wa kitengo cha kifua kikuu katika Hospitali ya wilaya kwa huduma nzuri ambazo zimesaidia kuokoa maisha yake na watu wengine.

Salum Jawabu mkazi wa Mchuruka aliyemaliza dawa za kifua kikuu na kupoma,amewaomba watu waliobainika kuwa na TB na kuanzishiwa matibabu kuendelea kumeza dawa badala ya kukimbia kwani kufanya hivyo ni hatari kwa maisha yao.

Alisema,ugonjwa huo unatibika kwa mgonjwa kumeza dawa kila siku na kuepuka kukimbilia kwa waganga wa tiba asili na tiba ambao hawana vipimo na tiba sahihi za ugonjwa wa kifua kikuu.


Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.