MKOA wa Ruvuma umeweka mikakati ya kuinua ubora wa Elimu na kuongeza Taaluma Kitaifa.
Akizungumza Afisa Elimu Mkoa wa Ruvuma Hakimu Mafuru amesema Mkoa wamejipanga katika ufuatiliaji wa utekelezaji wa Mtaala wa Elimu katika ngazi za Elimu za Halmashauri.
Amesema mikakati hiyo ni pamoja na kuhimiza na kufuatilia ufayikaji wa mitihani ya upimaji wa mara kwa mara kwa madarasa yote,kutoa ushauri wa Halmashauri kufanya urekebishaji wa ikama ya walimu.
Kuhimiza utoaji wa motisha kwa wanafunzi na walimu Shule na Halmashauri zinazofanya vizuri kwenye taaluma pamoja na kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa utoaji wa chakula kwa wanafunzi wawapo Shuleni wakati wa mchana.
Afisa Elimu ameelezea changamoto katika Sekta ya Elimu ikiwemo wazazi kuhamia Mashamabani mbali na Shule na kuacha wanafunzi peke yao hivyo husababisha kuwa utoro na kuacha masomo.
Amesema baadhi ya wazazi kutochangia chakula upungufu wa walimu hasa katika Shule za Msingi,Kutokuwa na Shule za bweni zinazokidhi mahitaji pamoja na upungufu wa miundombinu,samani na hosteli.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkao wa Ruvuma
Septemba 16,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.