MKUU wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Laban Thomasi, amewakaribisha wawekezaji wakubwa na wadogo kukamata fursa za uwekezaji zinazopatikana mkoa humo.
Ametoa wito huo wakati halfa ya uzinduzi wa filamu maalumu ya utalii na uwekezaji iliyofanyika katika uwanja wa Majimaji Songea, amesema Mkoa huo unao fursa mbalimbali za kiuchumi kama vile samaki wa mapambo ziwa nyasa, kilimo na madini mbalimbali
Kanali Thomas ameeleza malengo ya filamu hiyo ni kuwaonyesha wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali duniani fursa zilizopo mkoani humo pia kuonyesha vivutio vya utalii vya utamaduni na kihistoria.
“Niwakaribishe wawekezaji kuja kuwekeza kwenye mkoa wetu kwa kuwa fursa za uwekezaji zipo nyingi, nawakaribisha kuja kutembelea fursa za utamaduni na kihistoria, tunayo hifadhi ya Mwalimu Nyerere katika Wilaya ya Namtumbo pamoja Natunduru”alisema Thomas.
Hata hivyo amewahakikishia wawekezaji kuwa swala la miundo mbinu kwenye Mkoa huo unafikika kwa njia za lami katika Wilaya zote za Mkoa huo, eidha upo usafiri wa anga ambao ni wa uhakika kuja Songea pia kuna usafiri wa maji kupitia ziwa nyasa
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.