SERIKALI ya Awamu ya Sita , mwezi huu inatarajia kuanza ujenzi wa Madarasa mawili ya Awali ya Mfano kupitia Mpango LANNES yenye thamani ya shilingi Milioni 57.8 katika shule ya Msingi Ndilima, Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Awali Kamati ya Ujeenzi wa Mradi huo wameweza kukutana katika ofisi ya kata ya maposeni tarehe 05/09/2023 ikiongozwa na Mwakilishi wa Afisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mwl. Sothery Nchimbi ambaye ni Afisa Elimu Maalum idara ya Elimu Msingi ili kuzijengea uwezo Kamati za ujenzi kupitia Force Akaunti.
Ambapo katika maelezo yake Mwakilishi wa Afisa Elimu wa Msingi ambaye ni Afisa Elimu Maalum Halmashauri ya Wilaya ya Songea ameiomba Kamati ya ujenzi kuwa waaminifu na kushirikiana katika kufanikisha ujenzi wa Madarasa hayo.
" Tunafanya ujenzi kwa ajili ya kuwezesha watoto wetu na wajukuu wetu waweze kusoma katika mazingira mazuri kwa hiyo niwaombe ndugu wajumbe kufanya kutekeleza ujenzi huu kwa uaminifu na kwa kuzingatia ubora na kwa kuangalia mstabali wa maisha ya watoto wetu ambao ndio watakao soma katika Madarasa hayo na kwa kufanya hivyo tutakuwa tumetekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi katika uboreshaji Elimu ya Tanzania"
"Aidha namshukuru Mheshimiwa Rais, Daktari Samiah Suluhu Hassan Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha kwa ajili ujenzi wa miundo mbinu ya Elimu katika wilaya ya Songea Aidha nawashauri kamati kuepuke kufanya kazi kiurafiki kwani tutakwamisha ujenzi,na kusababisha kujenga chini ya kiwango au vinginevyo"
Pamoja na hayo Mwakilishi huyo wa Afisa Elimu alitoa nafasi kwa wataalamu kutoka ofisi ya Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ili kutoa ufafanuzi wa kitaalamu wa mambo yanayohusu ujenzi kwa lengo la kufanikisha ujenzi huo, Maafiasa hao walikua na haya ya kusema-;
Raymond Joseph Afisa Manunuzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea" Lengo la kushirikiana kamati hii pamoja na wajumbe tunahitaji kuweka uwazi wa mradi, lakini kama Afisa manunuzi nawashauri kamati ya mapokezi ya ujenzi huu kuwa na kitabu cha reja ambacho kitasaidia kuandika vifaa vyote vitakavyo nunuliwa sokoni na kutoka stoo kuelekea kwenye ujenzi ili kuepusha upotevu wa vifaa wakati wa ujenzi"
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.