MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama wamekagua mradi wa ujenzi wa sekondari ya Jenista Mhagama mradi ambao unatekelezwa katika kijiji cha Parangu Halmashauri ya wilaya ya Songea.
Katika kutekeleza mradi huo serikali ilitenga bajeti ya shilingi milioni 962 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 12 vya madarasa,mabweni matano na matundu 20 ya vyoo ambapo uongozi wa shule hiyo umewezesha miradi kutekelezwa na fedha kubaki ambapo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ameshauri fedha zilizobaki kutumika kukamilisha mradi wa bwalo uliopo katika shule hiyo.
Miongoni mwa vyumba vya madarasa vilivyojengwa katika shule ya sekondari Jenista Mhagama
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.