Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Balozi Dkt. Pindi Chana amezindua Mikakati miwili (2) ya Kutangaza Utalii Kanda ya Kusini inayotekelezwa kupitia Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW) katika hafla iliyofanyika mkoani Njombe.
Mhe.Balozi Dkt.Pindi Chana amebainisha kuwa katika kufungua utalii mwaka 2017 Serikali ilianzisha Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW) kwa lengo la kupanua wigo wa mazao ya utalii kijiografia kwa kuendeleza Sekta ya Utalii katika mikoa ya Kusini.
Waziri Balozi Dkt. Chana amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa maono makubwa ya kuibeba sekta ya Utalii nchini si tu kwa Filamu ya The Royal Tour bali kupitia miradi na programu mbalimbali za kimkakati ukiwemo REGROW.
Katika uzinduzi huo, Mhe Balozi Dkt. Chana ameongeza kuwa Mikakati hiyo miwili imeainisha hatua mbalimbali ziyaakazochukuwa ili kuchochea ukuaji wa shughuli za utalii katika Mikoa ya Kusini ikiwemo Mikoa ya Iringa, Njombe, Ruvuma, Rukwa, Katavi, Mtwara, Lindi, Songwe, Mbeya, na Morogoro.
"Ni matarajio yetu kuwa, utekelezaji wa Mikakati hii utaongeza idadi ya watalii wanaotembelea ukanda huu hivyo kunufaika na faida zitokanazo na shughuli za utalii ikiwemo ongezeko la ajira na fursa za uwekezaji, mapato ya Serikali na mapato ya mwananchi mmoja mmoja". Amesema Waziri Balozi Dkt. Chana
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.