MKOA wa Ruvuma umefanikiwa kutoa mabingwa wawili katika mchezo wa ngumi za ridhaa kitaifa uliofanyika Mkoa wa Manyara.Mchezo huo ulianza Septemba 7 hadi 12, 2020 na kuibua washindi wawili ambao wamepata medali mbili za fedha (Silver) na shaba.
Washindi hao ni Athanas Mgungusi ambaye ni Mhifadhi wa wanyamapori wa Maliasili Mkuzo mjini Songea ambaye amejishindia medali ya fedha na Hosea Thomas ni Mhtimu wa chuo kikuu shahada ya Elimu ambaye amepata medali ya shaba.Akitoa taarifa ya ushindi huo katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma,Afisa Michezo wa Mkoa wa Ruvuma Anzawe Chaula amesema ushindi huo ni mkubwa ambao haujawahi kutokea katika mkoa wetu
Amesema kutokana na ushindi huo mkubwa waandaji wa mchezo huo kitaifa wamependekeza kupeleka mabondia hao walioshinda kutoka Mkoa wa Ruvuma wapelekwe kwenye fainali ya kitaifa ambazo zinatarajia kufanyika Desemba 2020. Hata hivyo chaula amesema mabondia hao wamefika ofisi ya Katibu Tawala Mkoa ambaye ni Mwenyekiti wa Michezo Mkoa kwa lengo la kukabidhi ushindi.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Steven Ndaki amesema kupitia ushindi uliopatikana katika Mkoa wa Ruvuma imekuwa ni historia ambayo haikuwahi kutokea tangu kuanzishwa kwa Mkoa huo.
‘’Juhudi hii waliyoionesha nipo tayari kutoa msaada katika fainali zitakazofanyika Desemba mwaka huu ili kuwawezesha kupata ushindi katika Mkoa wetu’’.alisema Ndaki.
Mkoa wa Ruvuma kwa mara ya kwanza umetoa washindi wawili kitaifa kwa mchezo wa ngumi za ridhaa.
Imeandikwa na Farida Musa na Aneth Ndonde
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Septemba 21,2020
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.