Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema Serikali inaendelea na ujenzi wa barabara ya Njombe -Kibena-Madeke Lupembe kuelekea Mikumi Mkoani Morogoro ili kuunganisha Mkoa huo na mikoa ya kusini.
Akijibu swali Bungeni jijini Dodoma leo Mhandisi Kasekenya amesema Serikali inaendelea na mpango wake wa kukamilisha ujenzi wa miradi ya barabara inayojengwa katika mikoa mbalimbali nchini.
“Mhe.Spika ujenzi wa barabara ya Mikumi-Ifakara KM 109, umekamilika,Ifakara-Mbingu KM 62. 5 na Mbingu-Chita KM 37.7 ujenzi unaendelea, Chita-Kibena mkoa wa Njombe Serikali inaendelea kutafuta fedha za ujenzi”Amesema Mhandisi Kasekenya
Aidha Naibu Waziri alikua akijibu swali la Mhe. Mbunge Viti Maalum Neema Mgaya aliyetaka kujua ni lini Serikali itaanza kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya Njombe-Kibena-Madeke-Lupembe mkoani Morogoro.
Naibu Waziri Kasekenya amesema Serikali tayari imesaini mkataba wa ujenzi wa barabara sehemu ya Ifakara-Lupilo-Mtimbila KM 112 kwa kiwango cha lami kwa utaratibu wa sanifu jenga.
Barabara hiyo ni sehemu ya barabara ya Kidatu-Ifakara- Londo hadi Lumecha Mkoani Ruvuma yenye jumla ya urefu wa km 435.8
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.