MKOA wa Ruvuma ambao unaoongoza kwa uzalishaji wa mazao ya nafaka nchini,unatarajia kujenga maghala 28 yenye uwezo wa kuhifadhi tani 28,000 za nafaka.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema maghala hayo yanajengwa kupitia Wizara ya Kilimo ambapo kila ghala litakuwa na uwezo wa kuhifadhi tani 1,000 za nafaka.
Amesema kati ya maghala hayo,maghala tisa yatajengwa Halmashauri ya Madaba,Halmashauri ya Songea maghala 11,Manispaa ya Songea ghala moja na Namtumbo maghala saba na kwamba maghala hayo yanajengwa katika mwaka wa fedha 2022/2023.
“Mbali ya uzalishaji maeneo ambayo yamechaguliwa kujengwa maghala hayo yamezingatia uwepo wa miundombinu ya barabara na umeme,Mkoa wa Ruvuma tumepewa asilimia 50 ya maghala yote ambayo yatajengwa Tanzania bara’’,alisisitiza RC Thomas.
Hata hivyo amesema licha ya mradi wa maghala hayo,serikali kupitia mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) ilikuwa na ujenzi wa maghala 25 katika katika Halmashauri za Songea,Madaba na kwamba hadi sasa maghala Matano yamekamilika na mengine yapo katika hatua mbalimbali za ujenzi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.