MKOA wa Ruvuma unatarajia kupanda hekari laki moja za miti kibiashara kwa kipindi cha miaka kumi kuanzia mwaka 2015 hadi 2025.
Afisa Maliasili Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Afrikanus Challe amesema upandaji miti huo unatekelezwa katika maeneo ya serikali kuu,serikali za mitaa,vyuo na shule na kwamba Mkoa umekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha upandaji miti na utunzaji mazingira.
“Uhamasishaji huu unakwenda sanjari na utekelezaji wa kampeni ya kitaifa ya upandaji miti ambao unafanyika katika Halmashauri zote’’,alisisitiza.
Amesema katika msimu wa mwaka 2023/2024 Mkoa wa Ruvuma unatarajia kupanda miche ya miti Zaidi ya milioni nne na kwamba miti hiyo ni kwa ajili ya mbao, vyanzo vya maji na matunda.
Akizungumzia ufugaji nyuki,Afisa Maliasili huyo amesema uzalishaji nyuki katika Mkoa wa Ruvuma unakumbwa na changamoto mbalimbali zikiwemo wafugaji nyuki wengi kutokuwa utaalam wa ufugaji nyuki wa kibiashara hivyo kushindwa kufanya ufugaji nyuki wenye tija.
Changamoto nyingine amezitaja kuwa ni uchomaji moto kwenye misitu ambao hutokea mara kwa mara hasa kwenye miti ya miombo,ukosefu wa masoko ya uhakika unaosababisha wafugaji nyuki kutothamini ufugaji wao na ukosefu wa mitaji hasa katika suala la kupata mizinga.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.