• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MKOA wa Ruvuma ulivyodhamiria kupunguza udumavu na utapiamlo

Imewekwa kuanzia tarehe: January 25th, 2023

 KATIBU Tawala Mkoa wa Ruvuma Ndugu Stephen Ndaki ameongoza kikao cha Kamati ya Lishe Mkoa ambacho kimelenga kupokea majukumu na viashiria vya kupima utendaji kazi wa Kamati ili kupunguza udumavu na utapiamlo.

kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mipango Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma pia kimepokea taarifa ya utekelezaji wa mkataba wa Lishe kwa kipindi cha Julai hadi Septemba 2022.

Akizungumza kwenye kikao hicho Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma amelitaja chimbuko la mkataba wa lishe unaotekelezwa katika ngazi zote,kuwa umetokana na utafiti ambao ulifanyika mwaka 2017 ambao ulibaini mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ukiwemo Mkoa wa Ruvuma iliyoongoza kwa udumavu.

“Tulikuwa tunajiuliza mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ndiyo inaongoza kwa uzalishaji wa vyakula vya aina zote sasa tukawa tunajiuliza chakula ni kingi tumedumaa vipi’’,alisema Ndaki.

Amesema wakati utafiti huo umefanyika Mkoa wa Ruvuma kwenye udumavu ulikuwa na asilimia 42 ya udumavu hivyo kuwa juu ya udumavu wa kitaifa ambao ni asilimia 39.

Hata hivyo amesema Mkoa umekuwa unachukua hatua mbalimbali za kupunguza kiwango cha udumavu ambapo umefanikiwa kupunguza kiwango cha udumavu kwa asilimia moja kutoka asilimia 42 hadi 41 kiwango ambacho amesema bado kipo juu.

Amesisitiza kuwa udumavu unapowakumba Watoto chini ya miaka mitano unaathiri hadi ukuaji wa ubongo hivyo ametoa rai kwa wajumbe wa Kamati ya Lishe Mkoa wa Ruvuma kila mmoja kuwajibika kwenye eneo lake ili kutoa elimu endelevu itakayosaidia kupunguza udumavu na utapiamlo katika Mkoa na Taifa kwa ujumla.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr.Luois Chomboko  akizungumza kwenye kikao hicho amesema ili kukabiliana na changamoto ya udumavu tangu mwaka 2017,serikali iliamua kutoa mkataba wa utekelezaji wa afua za lishe.

Amesisitiza kuwa mikataba hiyo imekuwa inatekelezwa  na kwamba Septemba 30,2022,mkataba wa lishe awamu ya pili umesainiwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ambao unatekelezwa katika ngazi za mikoa na Halmashauri.

“Lishe ni msingi wa uchumi na maendeleo na afya ya binadamu,tupo katika utekelezaji wa Mpango Mkakati Jumuishi wa pili wa Taifa wa Lishe unaoanzia mwaka 2021 hadi 2026’’,alisema Dr.Chomboko.

Hata hivyo amesema serikali imeahidi kuchangia asilimia 10.5 ya utekelezaji wa mpango huo ambao ni sawa na shilingi bilioni 67.22 katika utekelezaji na kwamba fedha hizo zitakuwa zinatoka katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa na Mkoa.

Kwa upande wake  Mratibu wa Lishe Mkoa wa Ruvuma Neema Mtekwa amesema katika kukabiliana na utapiamlo na udumavu,Mkoa umetoa maelekezo kwa wakurugenzi ili elimu ya lishe iendelee kutolewa kwa jamii na Taasisi.

Mtekwa amesema shule zote zimeelekezwa kutumia unga ulioongezwa virutubisho,kulima mahindi na maharage lishe ili kuongeza upatikanaji wake na kwamba kupitia kikao cha Mkoa wazabuni wameelekezwa kupeleka mahindi lishe shuleni.

 

Kutokana na hali ya lishe na udumavu kwa watoto chini ya miaka mitano kuwa mbaya nchini,Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,aliagiza kuwepo kwa mkataba wa usimamiaji wa shughuli za Lishe baina yake na Wakuu wa Mikoa yote 26 ya Tanzania Bara.

Imeandikwa na Albano Midelo wa Kitengo cha Mawasiliano Serikali Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Januari 25,2023

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.