Mkoa wa Ruvuma umeingia mikataba 13 na wakandarasi yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni sita kwa ajili ya kutekeleza kazi mbalimbali za matengenezo ya barabara na ujenzi wa madaraja na makaravati.
Mgeni rasmi katika hafla ya kuingia mikataba hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas.
Meneja wa TARURA Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Wahabu Nyamzungu amesema mikataba hiyo ni utekelezaji wa hatua ya pili kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.
Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini TARURA Mkoa wa Ruvuma una mtandao wa kilometa 7146.22 ya mtandao mzima.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.