• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MKOA wa Ruvuma waongoza kitaifa utoaji chanjo ya UVIKO kwa asilimia 148

Imewekwa kuanzia tarehe: October 22nd, 2021

MKOA wa Ruvuma umeongoza kitaifa zoezi la utoaji chanjo ya UVIKO 91 kwa kutoa chanjo kwa watu 44,549 sawa na asilimia 148.5.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge wakati anafungua kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mpango wa jamii shirikishi na harakishi wa utoaji wa chanjo ya UVIKO 19 kilichofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.

“Nitumie nafasi hii kuwapongeza wanaruvuma kwa  mwitikio mkubwa ambao kwa hakika umesababisha Mkoa wetu umeongoza kitaifa’’,alisema Brigedia Jenerali Ibuge.

Amesema Mkoa wa Ruvuma ulianza rasmi utekelezaji wa chanjo kwa wananchi Septemba 22 hadi Oktoba 14 mwaka huu,ambapo Mkoa ulivuka malengo kwa kumaliza dozi 30,000 ulizopewa kwa awamu ya kwanza na kuongeza dozi nyingine ziada 14,000 hivyo kufikia dozi zaidi ya 44,000.

Hata hivyo amesema tayari serikali ya Tanzania imepokea dozi zaidi ya milioni moja za chanjo  ya UVIKO 19 aina ya sinopharm kwa ajili ya kuendelea kuwapatia wananchi wake chanjo ambapo Mkoa wa Ruvuma umeletewa dozi zaidi ya 31,000 ambazo zinatarajiwa kuanza kutolewa kwa wananchi Oktoba 25 mwaka huu.

Amewaagiza watendaji wa Halmashauri zote mkoani Ruvuma kuhakikisha wanasambaza chanjo haraka katika vituo vyote 298 vinavyotoa chanjo na kwamba wataalam wa afya watoe elimu ya chanjo ya sinopharm ili ifahamike vizuri kwa wananchi kabla ya kuamua kuchanja kwa hiari.

Kwa upande wake Mratibu wa Chanjo Mkoa wa Ruvuma Winbroad Mvile ameitaja chanjo ya sinopharm kuwa inatolewa mara mbili ili kukamilisha dozi na kwamba chanjo hiyo inatengeneza kinga dhidi ya UVIKO 19 kwa asilimia 95.

Akizungumzia mgawanyo wa chanjo hiyo kwa kila Halmashauri mkoani Ruvuma,Mratibu huyo amesema Mkoa umeletewa dozi zaidi ya 31,291 za sinopharm  ambapo Manispaa ya Songea imepewa dozi 5300,Tunduru 5300,Namtumbo 5300, Halmashauri ya Mbinga 3572,Nyasa 3572, Halmashauri ya Songea 3572,Mbinga Mji 3572 na Madaba 1103.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa  wa Ruvuma Dr.Jairy Kanga ametoa rai wananchi ambao hawakupata chanjo katika awamu ya kwanza kujitokeza  ili  Mkoa wa Ruvuma na Taifa kwa ujumla kufikia hatua ya kupata kinga kundi (Herd Immunity) ili kufikia asilimia 60 hadi 70  ya watu wawe wamepata chanjo.

Akizungumzia chanjo ya sinopharm,Dr.Kanga amewataja walengwa wa chanjo hiyo kuwa ni mtu yeyote mwenye umri wa kuanzia miaka 18 na kwamba chanjo hii pia inatolewa kwa akinamama wajawazito na wanaonyonyesha.

Hata hivyo amesema mtu yeyote ambaye hajachanja chanjo ya kwanza ya Jassen& Jassen  anaruhusiwa kupata chanjo ya pili ya sinopharm na kwamba chanzo zote ni salama na zina uwezo wa kujikinga na UVIKO 19 kwa asilimia 95.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Oktoba 22,2021

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.