• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MKOA wa Ruvuma waongoza tena kitaifa uzalishaji chakula

Imewekwa kuanzia tarehe: January 13th, 2021


MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Chritina Mndeme amewapongeza wakulima Mkoani Ruvuma kwa kuongoza mara mbili mfululizo kitaifa katika uzalishaji wa mazao ya chakula nchini.

Mndeme ametoa pongezi hizo wakati anafungua Kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa wa Ruvuma kilichofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea mjini Songea.

Akizungumzia muhtasari wa hali ya chakula na mavuno mkoani Ruvuma kwa mwaka 2019/2021.Mndeme amesema katika kioindi hicho mavuno yalikuwa ni tani 1,355,509  hali iliyoufanya Mkoa wa Ruvuma kuchukua nafasi ya kwanza kitaifa.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amesema katika kipindi cha mwaka 2019/2021  mahitaji ya chakula katika Mkoa ni tani 469,172 hivyo Mkoa una ziada ya tani 886.337 na kwamba Mkoa umeendelea kufanya vizuri  katika uzalishaji wa mazao ya Kilimo kwa mara ya pili mfululizo.

“Mafanikio haya ni matokeo ya wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kwa kuendelea kujituma katika shughuli za kilimo bila kulazimishwa na usimamizi mzuri wa maafisa ugani Ugani na viongozi wa Serikali”,alisema Mndeme.

Mdeme ameyataja mazao ya Ufuta,Mbaazi,na Soya kwa mwaka huu katika Mkoa Ruvuma yamefanyika kupitia mfumo wa stakabadhi  ya Mazao ghalani  hali ilisaidia kuingiza mapato ya zaidi ya shilingi bilioni 28.

Kati ya mapato hayo, Ufuta limeingiza zaidi ya shilingi bilioni 25,Soya zaidi ya shilingi bilioni moja na Mbaazi zaidi ya shilingi bilioni bili.

Mndeme amesema Mkoa unaendelea kushirikiana na Taasisi zingine za Serikali katika kusimamia zoezi la ununuzi wa Korosho kutoka kwa wakulima ambapo hadi sasa zimeuzwa kilo 14,826,644 zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 33.

Kwa mujibu wa Mndeme msimu wa Kilimo wa Mwaka 2020/2021 Mkoa umelenga kulima hekta 672,137 za mazao ya chakula na bustani na kuvuna tani 1,790,582 za mazao hayo.

Hata hivyo,amesema katika msimu wa mwaka 2020/2021  serikali itaendelea na mfumo wa bei elekezi wa kununua pembejeo za kilimo hususani Mbolea ya kupandia (DAP) na ya kukuzia (UREA),na Wizara ya Kilimo pamoja na Mamlaka ya Udhibiti wa Ubora wa Mbolea Tanzania(TFRA)imetoa bei elekezi kwa kila Wilaya.

Mkoa wa Ruvuma ni gwiji katika uzalishaji wa chakula nchini baada ya kuongoza katika uzalishaji kitaifa kwa miaka miwili mfululizo.

Imeandaliwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Januari 13,2021 

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.