• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MKOA wa Ruvuma watenga ekari 48,343.35 kwa ajili ya kilimo cha mkataba

Imewekwa kuanzia tarehe: October 27th, 2021

MKOA wa Ruvuma umetenga jumla ya  ekari 48,343.35 za ardhi kwa ajili ya kilimo cha pamoja na Mkataba kwa zao la Alizeti,Ufuta na Soya ikiwa ni mkakati wake wa kutaka kujitosheleza kwa mafuta ya kula.

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amesema hayo jana,wakati akifungua Mkutano wa wadau  wa kilimo uliohudhuriwa na Wakuu wa wilaya,Wakurugenzi wa Halmashauri,maafisa ugani na taasisi za fedha.

Aidha amesema, mkakati huo unakusudia na utasaidia  Taifa kuepuka kutumia  fedha nyingi kuagiza bidhaa hiyo nje ya nchi na kuinua vipato vya wakulima na Nchi kwa jumla.

Ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kutenga Sh.bilioni 2.2 kwa ajili ya ununuzi wa mbegu bora za Alizeti ambazo awali zilikuwa zikiuzwa na wafanyabiashara kwa bei ya Sh.35,000 kwa kilo.

Ibuge amesema,kupitia mpango huo sasa mbegu za alizeti  zitauzwa kwa bei ya Sh.3,500 kupitia wakala wa mbegu(Asa) sawa na asilimia kumi ya  bei ya awali  na kuwasihi wananchi wa mkoa wa Ruvuma kutumia fursa hiyo kuwekeza katika kilimo cha zao hilo.

Amesema,katika mkoa wa Ruvuma mahitaji ya mbegu za alizeti,soya na ufuta ni  kilo 310,222 na mbolea ni tani 1,662 ambapo kwa msimu wa kilimo 2021/2022 Halmashauri za mkoa huo zimepanga kulima ekari 12,570 kati ya ekari 48,343 zilizotengwa.

Amesema, ekari hizo zitahitaji tani 112  ambapo zao la ufuta mahitaji ni tani 21,soya tani 77 na alizeti tani 14,na kuzielekeza Halmashauri kuhakikisha zinawezesha upatikanaji wa mbegu na pembejeo hizo kwa wakati ili wakulima wasikwame.

Pia amesema, katika msimu wa kilimo 2021/2022 mkoa huo umejipanga kutekeleza mfumo wa kilimo cha pamoja na kilimo cha mkataba(Block Farming& Contract Farming) kwenye Halmshauri ambacho kinahusisha utengaji wa maeneo  kwa wakulima hulima eneo moja.

Amesema, kilimo hicho wakulima watapata huduma za ugani na urahisi wa upatikanaji wa pembejeo na masoko ambapo wahusika wa mpango huo ni Vyama vya Ushirika,wakulima,vikundi,taasisi mbalimbali za umma na binafsi na makampuni ya ndani nan je ya Nchi.

Kwa mujibu wa Jenerali Ibuge,Serikali ya mkoa imeridhia kilimo hicho cha mktaba kwa wakulima kinachohusisha makubaliano baini ya mkulima na kampuni au mtoa huduma ambaye atahusika kutoa pembajeo,huduma ya ugani na ununuzi wa mazao  kwa lengo la kuinua kipato.

Katika kikao hicho, Ibuge ameziagiza Halmashauri kwenda kuviwezesha vikundi vitakavyohitaji kuwekeza katika mazao hayo, na kuhakikisha wanatenga eneo angalau moja  kwa ajili ya taasisi ya utafiti wa kilimo(Tari) ambalo litatumika  kama shamba darasa na kuzalisha mbegu bora kwa mazao ambayo Halmashauri itaanza nayo.

Kwa upande wake Katibu Tawala msaidizi uchumi na uzalishaji Jeremiha Sendoro amesema, manufaa ya kilimo cha pamoja ni kutumia rasilimali  kidogo kama maafisa ugani wachache kuwafikia wakulima wengi na kalenda ya kuhudumia shamba huandaliwa kwa pamoja.

Sendoro ametaja faida nyingine, ni  usambazaji wa pembejeo hufanywa  kwa urahisi kwa kuwa mashamba yote yapo kwenye uelekeo mmoja na upatikanaji wa masoko ni rahisi kwa sababu mazao ukusanywa kwenye maghala au soko moja.



Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.