Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Juma Haji Juma amemkabidhi vifaa vya michezo Diwani wa Kata ya Matiri katika Halmashauri hiyo Mheshimiwa Mbwambo.
Vifaa vilivyokabidhiwa na Mkurugenzi huyo ni jezi seti mbili za jezi na mipira mitatu .Vifaa hivyo vya michezo ni ahadi ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo aliyoitoa kwa washiriki waliocheza ligi ya Kata ya Matiri.
Pia Mkurugenzi huyo ametoa jezi na mipira miwili kwa timu ya Kigo city iliyopo kata ya Kigonsera,Lengo kubwa likiwa ni kuimarisha afya ya akili na mwili, kuhamasisha michezo pamoja kuibua vipaji vipya katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.