MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ametoa rai kwa wananchi mkoani hapa kujitokeza kwa wingi kuhesabiwa ifikapo Agosti 2022.
Ametoa rai hiyo wakati anazungumza na wananchi wa Madaba wilayani Songea katika ziara yake ya kikazi aliyoifanya hivi karibuni.
RC Ibuge amelitaja zoezi hilo kuwa litawezesha Taifa kupanga mipango ya Maendeleo ya muda mfupi na mrefu kwa mstakabali ya maisha ya wananchi.
Hata hivyo amesema zoezi hilo linaenda sanjari na uwekaji wa anwani za makazi na postikodi ili tuwe na uhakika wa kufanikisha sense ya mwaka huu.
“Niwakumbushe kuwa mwaka huu tunafanya sensa ya watu na makazi Hivyo nawahimiza wananchi wote kujitokeza kuhesabiwa’’,alisema RC Ibuge.
Katika hatua nyingine RC Ibuge amewakumbusha wananchi kujikinga na VVU na UKIMWI ambapo amewaasa wazazi na walezi kuwaelimisha vijana wao dhidi ya janga hili.
Imeandaliwa Ofisi ya Habari Mkoa wa Ruvuma
Machi 9,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.