• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma aagiza, watumishi Tunduru wachukuliwe hatua

Imewekwa kuanzia tarehe: June 16th, 2021

MKUU wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, ameagiza wataalam wa Halmashauri ya wilaya Tunduru ambao wamesababisha Halmashauri hiyo kupata hati yenye mashaka kutokana na hoja za mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali(CAG) wachukuliwe hatua.

Brigedia Jenerali Ibuge ametoa agizo hilo  kwenye kikao cha Baraza la madiwani la Halmashauri hiyo, kilichokaa kwa ajili ya kujadili hoja zilizotolewa na mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/2020.Amesema, hoja zilizotolewa na CAG katika Halmashauri hiyo zimetokana na uzembe kwa baadhi ya wataalam wake kwa kutofuata sheria na kanuni za ukusanyaji mapato na matumizi ya fedha zinazopatikana kutoka kwenye vyanzo vyake vya ndani.

“kwa hoja zilizotolewa na mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali katika Halmashauri yenu kwa kiasi kikubwa zimetokana na uzembe wa watumishi, na hoja hizo zimekuwa zinajirudia  mwaka hadi mwaka  kwa hiyo dhahiri watumishi  hawataki kujifunza na kujirekebisha, badala yake wanafanya kazi kwa mazoea”amesema.

Mkuu wa mkoa amesisitiza kuwa,ni lazima watumishi  hao wawajibike na kuchukuliwa hatua  ili iwe fundisho kwa watumishi wengine wanaoshindwa kutekeleza  wajibu wao na kusababisha upotevu wa mapato na kuwepo kwa hoja za mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali.

Amesema, katika matokea ya ukaguzi wa hesabu kwa mwaka wa fedha ulioisha tarehe 30 Juni 2020 Halmashauri hiyo imefanya vibaya tofauti na miaka ya nyuma ambapo kwa miaka mitano kuanzia mwaka 2014/2015 hadi 2018/2019 imepata hati safi.

Amesema,  kupata hati yenye mashaka inatokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutofanyika kwa  marekebisho ya hati za madai yaliyofanyika kwenye mfumo wa ukusanyaji wa mapato bila ya kuwa na nyaraka toshelezi ambayo ni shilingi 1,232,598,827.

Alitaja sababu nyingine iliyosababisha Halmashauri kupata hati yenye mashaka ni kuwepo kwa maelezo yasiojitosheleza kuhusiana na madai yaliyopoteza zaidi ya shilingi  24,296,173.Amesema, Halmashauri ya Tunduru kupata hati yenye mashaka siyo jambo jema hasa kwa Halmashauri yenye sifa ya kufanya vizuri katika suala zima la maendeleo na kuagiza kila mmoja ahakikishe anawajibika ili Halmashauri hiyo iendelee kupata hati safi kama ambavyo imekuwa kwa miaka ya nyuma.

Hata hivyo, amewapongeza kwa namna wanavyoifanyia kazi taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali ambapo katika utekelezaji wa hoja na mapendekezo yaliyotolewa kwenye taarifa ya CAG  Halmashauri imefanikiwa kufunga hoja 98 kati ya 108 za miaka ya nyuma  hivyo kusalia hoja 8 kwa hesabu jumuishi.

Amesema, kwa upande wa mfuko wa pamoja wa afya(Health Basket Fund) Halmashauri imefunga hoja 20 kayi ya 25 za miaka ya nyuma na kusalia hoja 5 ambazo zipo kwenye utekelezaji.Aidha,katika ripoti ya mwaka 2019/2020 kati ya hoja 29 zilizotolewa hoja 19 zimefungwa na kubakiwa hoja 10  na kwa upande wa mfuko wa pamoja wa afya hoja na mapendekezo 6 yaliyotolewa,hoja 3 zimefungwa.

Amewataka,kujipanga kwa ajili ya ukaguzi unaokuja  na utendaji wa majukumu yao siku zote ulenge kuzingatia taratibu ili kuzuia hoja na siyo kuwa sehemu ya kuzalisha hoja za ukaguzi na kuwasihi madiwani kuwa  makini na kufuatilia utekelezaji wa hoja hizo.

Kwa upande wake Mkaguzi mkuu wa nje wa ofisi ya Mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za Serikali(CAG) mkoa wa Ruvuma Deogratius Waijaha ameshauri madiwani na watendaji wa Halmashauri hiyo, kufanya kazi kwa ushirikiano  ili kuwezesha kudhibiti  upotevu wa mapato.Amewataka watendaji katika Halmashauri  ya Tunduru kuhakikisha wanazingatia sheria za manunuzi,kanuni,taratibu pamoja na kusimamia matumizi ya mashine za EfdS pamoja na mfumo wa POS.

Imeandikwa na Muhid Amri,Mwandishi magazeti ya serikali

Juni 16,2021

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.