• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma afanya ukaguzi wa kushitukiza Manispaa ya Songea

Imewekwa kuanzia tarehe: May 29th, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amefanya ukaguzi wa kushitukiza katika mradi wa nyumba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea iliyogharimu zaidi ya  milioni 202.

Mndeme amesema ameamua kufanya ukaguzi huo kutokana na Halmashauri ya Manispaa hiyo kuitelekeza nyumba hiyo tangu ilipokamilika na kufunguliwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2016

Amesema madai ya kutoanza kutumia nyumba hiyo kwa sababu ya kukosa uzio,hayana msingi kwa kuwa serikali imetumia fedha nyingi katika ujenzi wa nyumba hiyo.

“Jengo hili limejengwa kwa thamani kubwa sana,milioni 202 mheshimiwa Rais angeweza kujenga zahanati mbili kubwa na kununua madawa,pia Mheshimiwa Rais kwa kutumia fedha hizo angeweza kujenga wadi mbili za mama na mtoto,lakini Rais aliamua kutoa fedha hizi ili Mkurugenzi apate makazi’’,alisisitiza.

Hata hivyo Mndeme amemwagiza Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma,kufanya uchunguzi ili kuona thamani ya fedha iliyojenga jengo hilo,mwaka 2016 kama zimetumika kwa usahihi.

Mkuu wa Mkoa amesikitishwa na kitendo cha jengo hilo kutotumika tangu kukamilika kwake miaka minne iliyopita ambapo amesisitiza madai ya kusema nyumba haijaanza kutumika kwa sababu  hakuna uzio hayana msingi.

“Ni watu wangapi wanaishi  na kufanyakazi katika nyumba ambazo hazina uzio,ninyi kama Manispaa kama kigezo muhimu ni nyumba kuwa na uzio mlitakiwa kuchukua hatua mapema’’,alisema Mndeme.

Hata hivyo amesema uzio ungeweza kuwekwa wakati mtu anaendelea kuishi  ambapo ametoa siku tatu kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea kuhamia kwenye nyumba hiyo.

Amezuia fedha nyingine isitumike kwa ajili ya ukarabati wa jengo hilo na kwamba ameagiza  kiasi cha shilingi milioni 20 iliyotengwa kwa ajili ya uzio, asiwekwe Mkandarasi badala yake uzio ujengwe kwa kutumia force account.

Awali akitoa taarifa ya mradi huo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa hiyo Philipo Beno amesema mradi huo ulitekelezwa kwa awamu nne  ambapo awamu ya kwanza hadi ya tatu ilijengwa na Mkandarasi Shada Investiment co.Ltd na awamu ya nne ilijengwa na Mkandarasi MS AMU Communication Ltd.

Kwa mujibu wa Beno,Mradi huo ulianza kutekelezwa mwaka 2013  na kukabidhiwa Manispaa ya Songea Julai 4,2017.

“Changamoto iliyosababisha nyumba hii kutokaliwa hadi sasa ni kutokuwa na uzio,lakini katika bajeti yetu ya mwaka 2018/2019,tuliweka bajeti ya ruzuku toka serikali kuu kiasi cha shilingi milioni 100 kwa ajili ya kumalizia uzio,ambayo hatukuipata’’,alisema Kaimu Mkurugenzi.

Hata hivyo amesema katika bajeti ya Manispaa inayoanzia Julai mwaka huu wametenga kiasi cha shilingi milioni 20 ili kujenga uzio huo.

IMEANDIKWA NA ALBANO MIDELO

AFISA HABARI MKOA WA RUVUMA

MEI 29,2020

SONGEA

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KIONGOZI mwenge wa Uhuru aonya rushwa kwenye uchaguzi

    May 10, 2025
  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.