• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma akemea mahubiri yanayoleta chuki

Imewekwa kuanzia tarehe: January 30th, 2024

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amekemea mahubiri yanayoleta chuki  na kuhatarisha amani na utulivu uliopo nchini.

Kanali Thomas ameyasema hayo wakati anazungumza na viongozi wa Taasisi mbalimbali za kidini mkoani Ruvuma kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.

Amewaasa viongozi wa dini kushirikiana na kuacha kudharauliana badala yake kujenga umoja wa madhehebu ya dini na kuzungumzia  changamoto na mafanikio waliyonayo kwa manufaa ya watanzania wote.

“Katika mahubiri yenu msisahau kuliombea Taifa letu,siasa zisiwagawe viongozi wa dini,tuangalia kwanza nchi yetu ya Tanzania,msikubali kuliingiza Taifa kwenye matatizo kisa Imani ya dini au vyama vya Siasa’’,alisisitiza RC Thomas.

Amesisitiza kuwa Tanzania ni moja na kamwe haiwezi kugawanyika kwa sababu ya migogoro ya kidini au kisiasa ambapo pia amewaomba viongozi hao wa dini  kuimarisha malezi bora kwa vijana na  ili kuwa na Taifa lenye maadili mema.

Ametahadharisha kuwa ndoa nyingi  zinavunjika kwa vijana ambapo amesema vijana wengi wanaingia kwenye ndoa bila kufanya maandalizi ya kutosha na kukosa mafundisho ya ndoa kutoka kwa viongozi wa dini.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa amewaomba viongozi wa dini kuwahimiza wazazi na walezi ambao bado hawajawapeleka Watoto wao shule wafanye hivyo mara moja.

Amesema kwa Watoto wanaosoma shule za serikali wanasoma bila ada na kwamba hata kama mtoto hana sare za shule wazazi na walezi wahakikishe wanampeleka mtoto  shule.

Akizungumza kwenye kikao hicho Askofu Noel Mbawala wa Kanisa la Upendo Masihi KIUMA wilayani Tunduru  ameipongeza serikali kwa kukemea mahubiri yaliyokuwa yanaleta uchochezi.

Amesema ili kuweka mahusiano mema Taasisi ya KIUMA  imeajiri watumishi wengi waislamu ili kuwa na amani na uhusiano ulio mwema ambapo ametoa wito kwa Taasisi nyingine za kidini kuiga mfano huo.

Hata hivyo ameiomba serikali kuchukua hatua  kwa vijana ambao wanatembea nusu uchi ambapo amedai msako wa kuwaondoa akina dada poa kutoka jijini Dar es salaam,wale akina dada wamerudi mikoani ambako wanaendeleza vitendo hivyo.

Amemuomba  Mkuu wa Mkoa  kwa kusaidiana na viongozi wa dini kuwakusanya akinadada hao ambao amedai wameingia mkoani Ruvuma ili kukaa nao na kuangalia namna ya kuwawezesha ikiwemo kuwapa mitaji midogo  na kupewa elimu ya biashara ili waaache  biashara haramu ya kujiuza.

Viongozi hao wa dini wamemuomba Mkuu wa Mkoa kushughulikia changamoto mbalimbali zikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya barabara katika baadhi ya mitaa mjini Songea, kudhibiti mgawo mkali wa  maji eneo la Misufini Mshangano na mlundikano wa takataka  katika eneo la Bombambili mjini Songea.

Mkuu wa Mkoa ameahidi kuzitafutia ufumbuzi changamoto zote ambazo wamezieleza ambapo amesema serikali ipo tayari kuendeleza ushirikiano na madhehebu ya dini ili kuwaletea maendeleo ya kimwili na kiroho.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma anaendelea na ziara ya kukutana na makundi mbalimbali ili kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.