• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma asisitiza upandaji miti

Imewekwa kuanzia tarehe: February 24th, 2023

MKUU wa mkoa wa Ruvuma kanali Laban Thomas amesema,suala la upandaji miti  katika wilaya zote tano za mkoa huo ni endelevu ili kusaidia kuhifadhi mazingira na vyanzo vya maji.

Laban ametoa agizo hilo kwenye uzinduzi wa zoezi la upandaji miti katika kijiji cha Kingerikiti kata ya Kingerikiti Halmashauri ya wilaya Nyasa,akiwa katika ziara ya kukagua miradi na shughuli mbalimbali za maendeleo wilayani humo.

Amewataka wananchi wa wilaya ya Nyasa,kuhakikisha wanaanzisha mashamba makubwa ya miti na anapanda angalau miti miwili kuzunguka maeneo yao kwani miti ni zao kubwa la biashara na lina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja,wilaya na mkoa wa Ruvuma.

Katika hatua nyingine Mkuu wa mkoa ameeleza kuwa,serikali ya awamu ya sita  kwa mwaka  wa fedha 2021/2022 imetoa zaidi ya shilingi bilioni 10 kupitia fedha za mpango wa maendeleo na mapambano dhidi ya Uvico-19 kujenga  vyumba vya madarasa  katika wilaya zote za mkoa huo.

Aidha amesema,mkoa huo  umepokea kiasi cha Shilingi bilioni 3.124 kwa ajili ya kujenga vyumba 110 vya madarasa ili kukabiliana na upunguzfu wa madarasa kwa shule za sekondari zilizopokea wanafunzi walioachaguliwa kuanza kidato cha kwanza kwa muhula wa masomo 2023.

Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa, mwaka 2022 mkoa wa Ruvuma umefanikiwa kujenga shule mpya za sekondari 11  katika Halmashauri zote nane za mkoa huo  kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 7.7,vyumba 792 vya madarasa kwa shule za msingi na sekondari vyenye madawati,viti na meza.

Hata hivyo alisema,jambo la kusikitisha licha ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali lakini bado kuna wazazi hawajui umuhimu wa elimu kwa kutopeleka watoto wao shule.

“mheshimiwa Rais anaangaika kutafuta fedha kwa ajili ya kujenga vyumba vya madarasa,lakini baadhi ya watu hawataki kupeleka watoto wao shule,sasa nawauliza mnataka wilaya yenu ya Nyasa kuwa na watu wa aina gani”alihoji Laban.

Alisema,serikali imejitahidi sana kutekeleza wajibu wake kwa kujenga vyumba vipya vya madarasa kila wilaya, kwa hiyo kilichobaki ni wazazi na jamii kuhakikisha watoto wao wanakwenda shule kupata elimu.

Edna Mahundi mkazi wa kijiji cha Kingerikiti,amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi zilizowezesha kujengwa kwa vyumba na shule mpya za sekondari wilayani Nyasa.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.