MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amevipongeza vyombo vya habari mkoani Ruvuma kwa kutekeleza ipasavyo wajibu wake kwa umma katika mapambano dhidi ya UVIKO 19.
Brigedia Jenerali Ibuge amesema vyombo habari vimechangia kutoa elimu kwa umma kuhusu chanjo ya UVIKO 19 hali iliyosababisha Mkoa wa Ruvuma kuongoza kitaifa kwenye utoaji chanjo kwa asilimia 148.
”Mnatoa huduma muhimu sana kwa jamii naomba muendelee hivyo kuwatumia wataalam wa afya kutoa elimu ya moja kwa moja kupitia vipindi vyenu ambavyo vinatoa fursa kwa wananchi kupiga simu na kupata ufafanuzi wa maswali mbalimbali “,alisema Ibuge .
Ametoa rai kwa vyombo vya habari vyenye vipindi vya kupiga simu kutoka wananchi na kuomba inapowezekana vipindi vitolewa bila gharama hali ambayo itaonesha moja ya uzalendo wa wanahabari katika masuala makubwa ya kitaifa kama mapambano dhidi ya UVIKO 19.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.