MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema katika mashindano ya ngoma za asili yaliyofanyika mkoani Mtwara ngoma ya mganda ya Boma la Mwenge kutoka Kata ya Kihagara Wilayani Nyasa na mwanamuziki Dula makabila walitia fora hivyo kuwa kivutio kwa wananchi wa kanda yote ya kusini
Kanali Thomas amesema hayo wakati anazungumza kwenye ufunguzi wa tamasha la mashindano ya ngoma za mganda katika kata ya Kihagara Wilaya ya Nyasa ambapo jumla ya maboma 17 yamealikwa kwenye mashindano hayo ambayo yanafanyika kwa siku mbili.
Mkuu wa Mkoa amewaagiza maafisa utamaduni wa Wilaya na Mkoa kuhakikisha wanasimamia usajiri wa vikundi vya utamaduni ili viweze kutambulika kisheria ili waweze kutumia sanaa kujiendeleza kiuchum
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.