Wananchi wa Kijiji Cha Mhangazi wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma waliandamana pamoja na kuamua kutojihusisha na shughuli zote za majitoleo Kwa ajili ya maendeleo ya Kijiji chao kutokana na kitendo Cha mwananchi wa Kijiji hicho kukamatwa kamatwa na kufunguliwa kesi za kuonewa.
Akiongea mbele ya mkuu wa wilaya ya Namtumbo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji hapo Lenatus Rufunda alisema anawashukuru wananchi wa Kijiji chake kuandamana mpaka ofisi ya mkuu wa wilaya baada ya kuona anavyoonewa kuhusu eneo lake ambalo alipewa na Kijiji Kwa kufuata utaratibu wa kisheria.
Akiongea Kwa masikitiko makubwa alimwambia mkuu wa wilaya hiyo kuwa amewahi kufungwa mara Tatu gereza la Songea Kwa kuonewa na mara ya Tatu wananchi wa Kijiji chake waliamua kuandamana pamoja na kususia shughuli za Maendeleo na ndipo aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyo Dkt Kenneth Ningu kulifuatilia jambo Hilo na kutolewa gerezani.
Mwenyekiti wa Kijiji Cha Mhangazi Alifa Mapunda alimwambia mkuu wa wilaya mpya kuwa vikao mbalimbali vimekaliwa kuhusu mgogoro wa mwananchi huyo kuonewa hata hivyo mlalamikaji alikuwa anamtengenezea kesi za jinai na kuacha mgogoro wa mashamba na kumfunga Kwa kuwa yeye ni askari mstaafu alisema mwenyekiti huyo.
Mapunda alidai baada ya wananchi wake kuona vitendo vya uonevu Kwa mwananchi mwenzao waliamua kuandamana mpaka Kwa aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyo Dkt Kenneth Ningu na kuwahaidi kulifanyia kazi na Kisha kumtoa gerezani .
Hata hivyo mwenyekiti huyo aliongeza kuwa askari huyo mstaafu anayefahamika Kwa jina la Oscar Wonanje mkazi wa Kijiji Cha Kitanda hataki kufuata utaratibu wa kupata maeneo badala yake anatumia nguvu na kuwatisha wananchi Kwa kutaka kuwaua Kwa kutumia silaha alisema mwenyekiti huyo.
Fidelis Gausi kaimu mtendaji wa Kijiji hicho alimwambia mkuu wa wilaya mpya kuwa eneo Hilo lilikuwa na msitu mkubwa lakini baada ya Kijiji kummilikisha Lenatus Lufunda akajitokeza huyo askari mstaafu na kumtaka Lenatus aache hiyo ardhi akidai kuwa eneo Hilo lilikuwa eneo waliokuwa wanaishi wazazi wao kabla ya kuanzisha Kwa operesheni ya vijijini mwaka 1974.
Fransis Mpalaza afisa ardhi wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo alifafanua kuhusu mpaka kati ya Kijiji Cha kitanda na Mhangazi kuwa ni mto Mhangazi kadiri ya Ramani na ofisi ya mkurugenzi ilishafika katika vijiji hivyo na kutafsiri Ramani hizo lakini Kijiji Cha kitanda wanaonekana kutokubaliana na Hilo.
MPalaza alidai kuwa mgogoro huo umepelekwa Kwa kamishna wa ardhi pamoja na migogoro mingine sugu Ili aweze kuitafutia ufumbuzi na kuondoa kero Kwa wananchi hao.
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Ngollo Malenya kupitia mkutano huo aliagiza eneo linalogombaniwa kati ya Lenatus Lufunda na Oscar Wonanje lisimame kufanyika kazi mpaka hapo ofisi yake itakapojiridhisha juu ya mgogoro huo.
Malenya alimwagiza mkuu wa jeshi la polisi wilaya ya Namtumbo kufuatilia Oscar Wonanje anayelalamikiwa kutaka kuwaua wananchi kuwa ni askari mstaafu kutoka jeshi Gani Ili waweze kuchukua hatua !
Mkuu wa wilaya aliwaambia wananchi kuwa askari anatakiwa kuwa mlinzi wa amani hata kama amestaafu lakini anaonekana ni kero kubwa Kwa wananchi alisema Malenya.
.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.