MKUU wa wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Ngollo Malenya anatarajia kuunda tume itakayoshughulikia kuchunguza malalamiko ya wananchi kuhusu uuzaji wa maeneo ya vijiji.
Malenya amefika uamuzi huo kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji Cha Songambele baada ya wananchi wa Kijiji hicho kuutuhumu uongozi wa Kijiji hicho kuhusika na uuzaji wa maeneo ya Kijiji hicho huku uongozi wa Kijiji hicho kukana kuhusika na uuzaji huo.
Mustafa Maleka mkazi wa Kijiji Cha Songambele alimwambia mkuu wa wilaya ya Namtumbo kuwa uongozi wa Kijiji hicho umehusika kuuza maeneo ya Kijiji bila kufuata utaratibu
Maleka Adam Maleka Naye mkazi wa Kijiji Cha Songambele alimwambia mkuu wa wilaya kuwa mwenyekiti wa Kijiji hatoi majibu sahihi kuhusu msitu uliouzwa na kuharibiwa wa Kijiji hicho.
Mzabuni Maleka Naye mkazi wa Kijiji Cha Songambele alidai mwenyekiti huyo alisimamishwa katika nafasi yake kutokana na tuhuma za kushindwa Kutoa majibu ya uuzaji wa maeneo ya Kijiji hicho , hivyo tunashangaa kumwona akiwa anaongoza mkutano tena alisema Maleka.
Mwenyekiti wa Kijiji Cha Songambele Omari Magazini alimwambia mkuu wa wilaya kuwa tuhuma zinazoelekezwa kwake na uongozi wake hazina ukweli wowote Bali familia ya Maleka ni familia iliyokuwa inajihusisha na tabia ya ki- Al- Shabab katika Kijiji hicho.
Magazini alisema wakati wa operesheni uliofanywa na Serikali kuhusu watu wanaojihusisha na tabia ya ki_ Al-Shabab Kijiji hicho Cha Songambele kilitaja familia hiyo kujihusisha na Al Shabab Hali iliyoibua chuki kwake .
Pamoja na hayo Mkuu wa wilaya alitoa nafasi Kwa viongozi na wananchi kuzungumzia tuhuma zinazomkabili mwenyekiti huyo ikaonesha baadhi ya wananchi kuunga mkono kuuzwa Kwa maeneo ya Kijiji hicho lakini baadhi ya wananchi kupinga kuuzwa Kwa maeneo hayo Kwa madai kuwa maeneo hayo yamevamiwa na wafugaji ambao hawana vibali ya kukaa katika maeneo hayo huku wengine wakidai viongozi wamewauzia.
Kufuatia sintofahamu hiyo mkuu wa wilaya ya Namtumbo aliwaambia wananchi hao kuwa ataunda tume ya kuchunguza malalamiko hayo Ili viongozi wanaokumbatia wafugaji wakibainika kufanya hivyo kutoka kwenye taarifa ya tume watashughulikiwa .
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.