MKuu wa Wilaya ya Nyasa Mheshimiwa .Filberto Sanga amesema Serikali Kwa kushirikiana na wananchi wa Kata ya Linga itatatua changamoto ya ukosefu wa shule ya Sekondari na mawasiliano ya mtandao wa Simu za mikononi.
Ameyasema hayo hivi karibuni wakati akiongea na wananchi hao katika Viwanja vya mikutano uliofanyika katika Kijiji Cha Ngingama kata ya Linga Wilayani hapa.
Mheshimiwa .Sanga amefafanua kuwa amefika katika kata ya Linga Kwa lengo la kuwatembelea wananchi, kutangaza kazi za Serikali na kusikiliza na kutatua kero Za wananchi, hivyo ameona uhalisia kuwa Moja ya changamoto zinazowakabili wananchi ni ukosefu wa shule ya Sekondari na mawasiliano ya mitandao ya Simu.
Ameongeza kuwa kata hiyo ni kata pekee Wilayani Nyasa ambayo Haina Sekondari ya kata, na wanafunzi wanatembea umbali mrefu kufuata Sekondari ya Lituhi, Hali ambayo inawakwaza wanafunzi kutopenda masomo au kusababisha utoro na kushuka kiwango Cha elimu.
Amesema changamoto nyingine ni ukosefu wa mawasiliano ya mtandao wa Simu, za mikononi hivyo amewaomba wananchi kuwa wavumilivu na Serikali itahakikisha inatatua changamoto hizo.
"Serikali itahakikisha inatatua changamoto ya ukosefu wa shule ya Sekondari na mawasiliano ya mtandao wa Simu za mikononi,Kwa kuwa Ninashirikiana vema na mbunge wa Jimbo la Nyasa mhandisi Stella Manyanya kutatua changamoto hizi hivyo wanalinga muwe na subira wakati Serikali inajipanga kutatua changamoto hizi"
Awali wananchi walisema tayari wanaeneo la kujenga shule ya Sekondari na wako tayari kuchangia Ujenzi huu wa shule ya Sekondari,Kwa hiyo wameiomba Serikali kutatua changamoto hii ili kata ya Linga iwe na Maendeleo.
Aidha wameipongeza Serikali Kwa kutatua changamoto ya maji, Barabara, na mradi wa shule ya msingi muhurasi na vyoo vya shule ya msingi Ngingama.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.