• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MKUU wa Wilaya ya Tunduru awaonya wanaume

Imewekwa kuanzia tarehe: May 15th, 2023

MKUU wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Julius Mtatiro,ameiagiza Halmashauri ya wilaya hiyo kukamilisha haraka mchakato wa kutunga sheria ndogo itakayobana wanaume wenye tabia ya kuwachelewesha wake zao wajawazito kufika katika vituo vya afya kwa wakati.

Mtatiro ameyasema hayo jana wakati,akizindua wiki ya chanjo kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano na wasichana wenye umri wa maiaka 14 katika zahanati ya Mapambazuko inayomilikiwa na Kanisa Katoriki Jimbo la  Tunduru-Masasi.

Alisema,serikali kupitia wizara ya afya imeweka utararibu wa mama  anapohisi mjawazito kuwahi kliniki mapema wakati wote wa ujauzito na hata baada ya kujifungua ili kuangalia maendeleo ya afya zao.

Alisema,chanjo inasaidia kuwakinga wajawazito na hatari ya kupata magonjwa na kwa watoto wanaozaliwa  kuwa na kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali yanayozulika ikiwemo surua,kupooza,kifua kikuu na kifaduro.

Alisema,kuna watu wanapotosha ukweli kuhusiana na umuhimu wa chanjo ikiwemo chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 14 walioko shuleni na majumbani kwa kueleza kuwa,ina madhara jambo ambalo  halina ukweli.

“chanjo hii ni muhimu sana kwa ajili ya watoto wetu waliopo shule na wale walioko nyumbani,nawaomba wazazi hasa akina mama msikubali kuwasikiliza wapotoshaji,changamkieni chanjo  ili kuwaokoa watoto wenu na hatari ya kupata ugonjwa huo”alisema.

Mtatiro amewataka akina mama,kuhakikisha wanakula chakula chenye virutubisho vyote muhimu ili kujenga familia zenye afya bora,badala ya kula chakula cha aina moja kila siku ambacho kinaweza kusababisha  tatizo la udumavu na utapiamlo kwa watoto wao.

Amewahimiza wananchi,kuhakikisha wanazingatia na kufuata ushauri unaotolewa na wataalam wa afya ili kujikinga kupata maambukizi ya magonjwa mbalimbali  yanayoweza kuepukika.

Katika hatua nyingine,Mtatiro amewakumbusha wananchi juu ya kutunza na kujiwekea akiba ya chakula wanachozalisha kwa ajili ya matumizi ya familia zao na kuepuka tabia ya kuuza chakula chote kutokana na tamaa ya kupata fedha.

Alisema,serikali haitakuwa tayari kutafuta chakula cha msaada kwa watu waliofanya uzembe wa kuuza chakula walichazalisha na kusahau kuweka akiba kwa matumizi  yao.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa wilaya hiyo Dkt Wilfred Rwechungura alisema,kampeni hiyo imelenga kuwatafuta na kuwafikia kwa wakati watoto wote wanaostahili kupata chanjo hizo ili watoto na akina mama wa Tunduru wanakuwa salama.

Alisema,chanjo hiyo ni muhimu ili kuhakikisha watoto wanakuwa na afya njema na kuwakinga na magonjwa yanayoweza kuzuilika.

Dkt Rwechungura ametoa wito kwa wazazi na jamii kwa ujumla, kutoa ushirikiano kwa wataalam  waliopo na watakaofika katika maeneo yao ili waweze kutoa huduma hiyo muhimu.

Awali mratibu wa chanjo wilaya ya Tunduru Rose Jemeni alisema,lengo la wiki ya chanjo ni kuwapatia watoto wote na wasichana wenye umri wa miaka 14 ambao hawakupata au hawajakamilisha chanjo kulingana na ratiba ya chanjo.

Alisema,lengo ni kuwakinga na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo na kuelimisha jamii juu ya umuhimu wake katika kuokoa maisha na kuboresha uchumi na zoezi la hilo litafanyika kwenye vituo vyote vya kutolea huduma kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 11 jioni.

Alisema,tangu kuanza kwa mpango wa chanjo kwa watoto kumekuwa na mafanikio mbalimbali ikiwemo kupungua kwa magonjwa yanayozulika kwa chanjo na jamii kufahamu umuhimu wake.


Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.