KUKWAA la Wanawake Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma limezinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mheshimiwa Julius Mtatiro likiwa na lengo la kuwapa fursa na kuwapambania wanawake waweze kujiimarisha kiuchumi na kujikwamua na kipato duni.
Akihutubia Jukwaa hilo Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mheshimiwa Julius Mtatiro, alisema Jukwaa hili likiwezeshwa kikamilifu litakua msingi wa kutatua changamoto mbalimbali, kwasababu katika falsafa ya uchumi mwanamke ana uwezo mkubwa wa kutunza Fedha, ni vyema kuwepo na uchumi shirikishi ndani ya familia.
“Jukwaa hili halijazinduliwa kwa maamuzi ya mtu mmoja, uundwaji wake ni maagizo ya mikataba mbalimbali pamoja na sheria ambazo zinalinda maslahi ya mwanamke wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali inapinga vikali ndoa za utotoni, Binti aachwe asome”. Alisema.
Kwa upande wake Katibu wa jukwaa la wanawake Mkoani Ruvuma Mwl. Neema Kajange alisema, Mama ni mlinzi mkubwa wa familia na ili kumfikia mwanamke wa chini kabisa Halmashauri zitenge kifungu kitakachosaidia kuwaunganisha na kushiriki katika majukwaa yanayohamasisha shughuli za uchumi na uzalishaji mali.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.