• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MRADI wa daraja la Ruhuhu wakamilika kwa asilimia 100

Imewekwa kuanzia tarehe: February 25th, 2022

WAKALA wa Barabara nchini(Tanroads) imepiga hatua nyingine, baada ya kukamilisha ujenzi wa daraja la urefu wa mita 98 katika mto Ruhuhu linalounganisha wilaya ya Nyasa mkoa wa Ruvuma na Ludewa mkoa wa Njombe .Baadhi ya wahandisi wa Tanroads kutoka mikoa mbalimbali nchini walioshiriki kujenga daraja hilo walisema, kukamilika kwa daraja hilo ambalo limejengwa kwa ubora wa hali ya juu na wahandisi wa Kitanzania ni mafanikio makubwa kwa Serikali ya awamu ya sita.


Mhandisi Mwandamizi wa Tanroads Makao makuu Secilia Kalangi alisema, daraja la Ruhuhu limejengwa kwa vyuma badala ya zege na wataalam wa Kitanzania kutoka mikoa 26 ya Tanzania kwa kushirikiana na wataalam wa Tanroads makao makuu.

Kalangi alisema, daraja limekamilika kwa asilimia mia moja na ameipongeza wakala wa Barabara nchini( Tanroads) kuwaamini waandisi wake ambao walifanya kazi usiku na mchana kuhakikisha ujenzi wa mradi huo muhimu kwa uchumi unakamilika kwa wakati.

Kalangi ambaye alikuwa kiongozi wa Timu ya waandisi hao, ameishukuru Wizara ya Ujenzi kuwapa dhamana ya kutekeleza mradi huo mkubwa ambao ulikuwa unasubiriwa kwa hamu na wananchi wa mikoa hiyo miwili.

Alisema, hatua ya serikali kuwatumia wahandisi wa ndani imesaidia kuokoa fedha nyingi kama ingewatumia wakandarasi wa nje,pia daraja hilo limetumika kama sehemu ya mafunzo kazini kwa waandisi wazalendo katika kujenga madaraja ya aina hiyo ambayo ni machache hapa nchini.

Aidha alisema, sehemu hiyo ilikuwa shida kupitika kutokana na kuwepo kwa wanyama wakali hasa mamba na viboko ambao walitishia na kupoteza maisha ya wananchi wengi walipotaka kuvuka kutoka upande mmoja kwenda mwingine.

Ndiyo maana,serikali iliamua kujenga daraja kutokana na changamoto ya usafiri kati ya mkoa ya Ruvuma na Njombe na baada ya kukamilika limerudisha matumaini kwa wananchi wa mikoa hiyo ambao wameanza kufurahia matunda ya Serikali yao.

Mhandisi Vicent Shirima kutoka Tanroads mkoa wa Njombe, alitaja fursa zinazoweza kupatikana baada ya kukamilika kwa daraja ni pamoja na kusafirisha makaa ya mawe yanayochimbwa kwa wingi wilaya ya Ludewa kwenda Bandari ya Mtwara .Shirima alitaja manufaa mengine ni kuwawezesha wakulima,wafanyabiashara na wananchi kusafirisha mazao na bidhaa zao kwenda katika mikoa mbalimbali nchini kutafuta masoko na amewataka kutumia daraja hilo kuongeza uzalishaji na kufanya biashara,badala ya kuacha fursa hiyo ikiwanufaisha watu kutoka nje ya mkoa huo.

Naye Mkuu wa kitengo cha mipango Tanroads mkoa wa Ruvuma Msama Msama alisema,daraja hilo linatimiza adhima ya Tanroads kuunganisha watu wa sehemu moja na nyingine, kukuza uchumi na kuharakisha maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Nchi kwa ujumla.

Alisema,daraja la Ruhuhu limejengwa katika nguzo kuu nne zilizobebwa na msingi wenye nguzo nyingine ndogo(Piles)48 na umegharimu jumla ya Sh.8,976,808,037.64.

Kwa mujibu wa Msama, baada ya kukamilika kwa ujenzi huo kilichobaki ni wananchi wenyewe kutumia fursa hiyo kusafirisha bidhaa kwani limekuwa mkombozi mkubwa kwao.

Amewataka,wananchi wanaoishi vijiji jirani vya Lituhi kwa upande wa Nyasa na Kipingu Ludewa kulinda daraja hilo kwa kuwa ni mkombozi mkubwa kwao, hivyo lazima walilinde kwa gharama yoyote ili liwasaidie katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na kutambua kuwa Serikali imetumia fedha nyingi.

Kwa upande wake Mhandisi Geroge Nyagaboma kutoka Kilimanjaro alisema,watatumia ujenzi wa daraja la Mto Ruhuhu kama sehemu ya mafunzo kazini kwa kujenga madaraja mengine hapa nchini kwa weledi mkubwa.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kipingu kata ya Manda wilayani Ludewa Elasmus Mbeya,amefurahishwa na hatua ya Serikali kukamilisha mradi huo ambao umerahisisha mawasiliano kati ya mkoa wa Njombe na Ruvuma ambayo inategemeana katika mambo mbalimbali ya kiuchumi na kijamii.
MWISHO.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.