• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MRADI wa maji miji 28 utakavyowanufaisha wananchi Songea

Imewekwa kuanzia tarehe: January 30th, 2025

Katika juhudi za kuboresha huduma za maji safi na usafi wa mazingira, serikali ya Tanzania imeanzisha Mradi wa Maji wa Miji 28, ambao unatekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Mji wa Songea mkoani Ruvuma ni miongoni mwa miji inayonufaika na mradi huu, kwa lengo la kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wake.

Mkurungezi wa Mamlaka ya Maji safi Songea (SOUWASA) Mhandisi Patrick Kibasa anasema Mkataba wa mradi huu ulisainiwa tarehe 10 Machi 2023 kati ya Wizara ya Maji na China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) kwa gharama ya TZS Bilioni 145.77.

Anasema Utekelezaji wa ujenzi ulianza rasmi tarehe 2 Januari 2024, na hadi sasa maendeleo yamefikia asilimia tano

Kulingana na Kibasa Mradi huu umebuniwa ili kuongeza upatikanaji wa maji na kuboresha miundombinu ya maji safi kwa wakazi wa Songea ikiwemo Ujenzi wa miundombinu ya kudaka maji kutoka Mto Njuga katika kijiji cha Kikunja, Halmashauri ya Wilaya ya Songea.

Anasema mradi  huo utaongeza uzalishaji wa maji hadi lita milioni 17 kwa siku.

Kibasa anasema mradi huo unahusisha Ujenzi wa matanki matatu ya kuhifadhi maji yenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni 9. Ujenzi wa matanki haya tayari umeanza na Ujenzi wa mtandao wa bomba za usambazaji maji wenye urefu wa 34.7 km ili kuwafikia wakazi wengi zaidi wa mji wa Songea.

“Mradi pia unahusisha Ujenzi wa mtambo wa kisasa wa kuchuja na kusafisha maji wenye uwezo wa kuchakata lita milioni 16 kwa siku, ili kuhakikisha maji yanakuwa safi na salama kwa matumizi ya binadamu”.anasema Kobasa Anaongeza kuwa mradi pia unahusisha Ukarabati wa mtambo wa kuchuja na kusafisha maji wa Matogoro, wenye uwezo wa lita milioni 11.5 kwa siku, ili kuboresha huduma za maji safi kwa wakazi wa Songea.

Anazitaja faida za Mradi huo kuwa ni pamoja na kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya maji katika mji wa Songea. Baadhi ya faida zake ni pamoja na:

Kuongeza idadi ya watu wanaopata maji safi na salama, kutoka asilimia 90 hadi 95 au zaidi,Kuboresha ubora wa maji, kutokana na uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya kisasa ya kuchuja na kusafisha maji na Kuimarisha usafi wa mazingira, hivyo kupunguza magonjwa yanayotokana na maji

Mradi wa maji wa mji wa Songea ni sehemu muhimu ya mkakati wa kitaifa wa kuboresha huduma za maji safi na usafi wa mazingira.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBINGA-MBAMBABAY : barabara inayojenga utalii kwenye milima ya Kusini

    June 01, 2025
  • PICHA ya Rais Samia yapamba mti wa kihistoria Namtumbo

    June 01, 2025
  • TAIFA lamlilia Songambele Shujaa wa Uhuru aliyeishi karne moja

    June 01, 2025
  • SHAMBA la AVIV Tanzania ni mfano wa kuigwa nchini

    June 01, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.