• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MRAJISI atoa rai kwa wadau kujifunza mfumo wa stakabadhi ghalani mkoani Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: May 14th, 2021

Mrajis wa vyama vya Ushirika Nchini Dkt Benson Ndiege amewataka Viongozi,wanachama  wa Ushirika na wakulima kuja kujifunza soko la mfumo wa stakabadhi ghalnani mkoani Ruvuma kwasababu Mkoa umefanikiwa katika kusimamia na kuendesha soko hilo.

Dkt Ndiege ametoa kauri hiyo wakati akishuhudia ufunguzi wa soko la pili la mnada wa kitaifa wa mazao yanayouzwa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani uliofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma hivi karibuni.

Dkt Ndiege amesema mkoa wa Ruvuma umefanikiwa katika kuelimisha wakulima na kuwaunganisha pamoja katika soko la mfumo wa stakabadhi ghalani,hivyo amewataka Viongozi,wanachama wa Ushirika na wakulima kufika Ruvuma kujifunza juu ya mfumo huo.

 “Nyie Songea au Ruvuma ni mfano mzuri kwenye mfumo wa stakabadhi ghalani nawapongeza”,amesema Dkt Ndiege.

Amesema mfumo wa stakabadhi ghalani ni mfumo shirikishi kwa wakulima na wafanyabiashara ambao unatoa fursa kwa wakulima kukusanya na kuuza mazao yao kwa pamoja na kutatua changamoto za ukosefu wa soko la uhakika vilevile humpunguzia mnunuzi gharama za ufuatiliaji na uhakika wa kupata mazao yenye ubora.

Amewataka wafanyabiashara kujali maslahi ya wakulima kwa kununua mazao hayo kwa bei ambayo hai mkatishi tamaa mkulima katika kuendelea kuzalisha zao hilo ambalo uzalishaji wake ni mgumu ukilinganisha na mazao mengine.

Kwa upande wake Afisa shughuli wa chama kikuu cha Ushirika cha SONAMCU Zamakanaly Komba amesema katika soko la mfumo wa stakabadhi ghalani wakulima ndiyo mtaji katika kuendesha soko hilo na wanamamlaka ya kukubali au kukata kuuza mazao yao endapo bei inyotajwa kutokuwa na maslahi kwao.

Komba amesema kwa msimu wa kilimo wa mwaka 2020/2021 katika soko la kwanza la mnada jumla ya tani 164 zilikusanywa toka kwa wakulima kupita Vyama vya Msingi vya Ushirika ambapo wakulima walikata kuuza kutokana bei kutowaridhisha ya shilingi 2210 kwa kilomoja.

Kwa upande wa wakulima wamedai bei hiyo ni ndogo wametaka wastani wa bei ianze na shilingi 3000 hadi shilingi 2500 kwa kilomoja ambayo inamaslahi kwao kulinga na gharama za uzalishaji.

Naye afisa kilimo wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Hellen Shemzigwa amesema kwa msimu wa kilimo wa mwaka 2021/2022 Halmashauri inatarajia kuuza taani 2600 za ufuta.

Mfumo wa stakabadhi ghalani katika mkoa wa Ruvuma umewaingizia wakulima zaidi ya kiasi cha shilingi bilioni 28 kwa mazao ya ufuta,soya,na mbaazi  katika msimu wa masoko wa mwaka 2020/2021.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.