Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Pololet Mgema amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Madaba kwa kushirikiana na watendaji wa kata kuanza msako wa nyumba kwa nyumba kuwatafuta wanafunzi wa sekondari ambao hadi sasa hawajaripoti katika shule walizopangiwa
Akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la madiwani Halmashauri ya Madaba Mheshimiwa Mgema ameagiza hadi kufikia mwishoni mwa Januari mwaka huu wanafunzi wote wawe shuleni.
Awali akitoa taarifa ya mahudhurio ya wanafunzi wa sekondari,Afisa Elimu Sekondari Maternus Ndumbaro amewataja jumla ya wanafunzi 1269 walipangwa katika shule za sekondari kuanza kidato cha kwanza ambapo hadi kufikia Januari 19,2023 ni wanafunzi 535 ndiyo wameripoti sawa na asilimia 42 ambapo asilimia 58 ya wanafunzi bado hawajaripoti.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.