Watu Sita wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, Leo Desemba 28, 2024.
Waliopoteza maisha katika ajali hiyo iliyohusisha gari ndogo aina ya Prado ( T 647 CVR ) ni walimu wanne wa shule ya msingi Lumalu, dereva wake aliyefahamika kwa jina la Vicent Alel Milinga pamoja na Raia mmoja.
Mkuu wa wilaya ya Nyasa Mheshimiwa , Peres Magiri amethibitisha idadi ya vifo hivyo vilivyosababishwa na ajali hiyo iliyotokea wakiwa njiani kutoka kijiji cha Lumalu kilichopo katika Kata ya Upolo kuelekea makao makuu ya wilaya.
Walimu waliopoteza maisha ni Damas Damasi Nambombe, Domenica Abeat Ndau, Judith Joseph Nyoni na John Silvester Mtuhi.
Raia aliyefariki dunia ni Boniface Bosco Mapunda.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.