Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Julius S. Mtatiro amemkabidhi ofisi Mkuu wa Wilaya Tunduru Mhe. Simon K. Chacha na kumueleza changamoto ambazo anatakiwa kuzifanyia kazi.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Tunduru na kuhudhuriwa na wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na viongozi mbalimbali kutoka Wilaya ya Tunduru.
Mhe. Mtatiro amewaomba Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya na Watumishi wa Halmashauri ya Tunduru kumpa ushirikiano Mkuu Wilaya ya Tunduru Mhe. Chacha.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe. Simon Kemori Chacha, amempongeza Mkuu wa Wilaya aliyetangulia na kusema atayaendeleza yale ambayo yaliachwa na Mkuu wa Wilaya huyo.
Kufuatia Uteuzi na mabadiliko ya Chacha kabla ya kuhamia Tunduru alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora na Mtatiro amehamishiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.