• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MWAMBESI msitu wa hifadhi wenye ndege waliohamia toka Madagascar

Imewekwa kuanzia tarehe: May 24th, 2024

MSITU wa Hifadhi wa Taifa wa mazingira asilia Mwambesi uliopo wilayani Tunduru mkoani Ruvuma ulianzishwa mwaka 1956 na ulipandishwa hadhi kuwa msitu wa Taifa katika kipindi cha mwaka 2017/2018.

Meneja wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Denis Mwangama katika wilaya ya Tunduru anasema msitu huo umepandishwa hadhi ili kuongeza uhifadhi zaidi kutokana na kuwa na utajiri wa viumbe vya kipekee duniani wakiwemo wanyama,ndege na mimea.

Anawataja wanyama waliopo katika msitu huo ambao upo kando kando mwa Mto Ruvuma kuwa ni simba, tembo, chuo,kuro,jamii za nyani,jamii za swala,nyati na wanyama wengine.

Mwangama anasema Katika msitu wa Mwambesi kuna jamii ya ndege maarufu duniani anayeitwa Pentiole ambaye utafiti uliofanywa na PALMS Foundation mwaka 2015 umebaini kuwa ndege huyo amehamia kutoka nchini Madagaska baada ya mazingira aliyokuwa anaishi kuharibiwa na shughuli za kibinadamu.

Kwa mujibu wa Mwangama, ndege huyo ana tabia ya kuzamia samaki kutoka majini na kwamba ndege hao wanapenda kuishi kwenye maporomoko ya  Mto Ruvuma yanayoitwa Sunda ambayo yapo ndani ya hifadhi hiyo.

“Tanzania tuna bahati katika msitu wetu tuna ndege Pentiole ambaye  amekuwa akiishi ukingoni mwa maporomoko ya maji yajulikanayo kama Sunda Water falls’’,anasisitiza.

Kwa mujibu wa Mwangama Ndege huyu huogolea kulingana na mawimbi ya maji yadondokayo kwenye maporomoko hayo akitatafuta mawindo yake ya samaki maana ndicho chakula chake pekee.

Licha ya ndege huyo Mwangama anayataja maporomoko ya Sunda kuwa ni miongoni mwa vivutio vya utalii katika hifadhi ya Mwambesi na kwamba maporomoko hayo yalitumika wakati wa vita ya  Majimaji kati ya mwaka 1905 hadi 1907 ili  kujificha kwenye mapango kwa juu.

Mto huu ndio uliokuwa ukitumika kwenye vita vya Majimaji ambapo watu wa makabila ya Ukanda  wa Kusini hususani  Wangoni walitumia maji yake katika kuzimia silaha za moto chini ya uongozi wa Kinjeketile Ngwale.

Pia eneo hilo linaaminika Wajerumani walitumia kama njia kubwa wakitokea Msumbiji katika biashara ya meno ya Tembo na Waarabu walipita pembezoni  mwa mto huo  kuwapitishia watumwa.

Hata hivyo anasema awali kabla ya serikali kuamua msitu huo kuwa Msitu wa hifadhi,kulikuwa na vitalu vya uwindaji wa kitalii ambapo ndani ya msitu kulikuwa na kambi ya wawindaji iliyoitwa Big Game ambayo ilikuwa na   Kampuni ya  uwindaji iliyoitwa Tandara Hunting Safaris.

Kulingana na Meneja huyo,msitu huo una ukubwa wa zaidi ya hekta 112,000 na kwamba umbali toka Tunduru mjini hadi ofisi za msitu huo ni kilometa 90.

“Msitu huu upo kando kando mwa Mto Ruvuma ambao pia unafanya mpaka wa asili kwa upande wa kusini magharibi mwa  msitu,kupitia mto Ruvuma kuna fukwe nzuri ambazo ni kivutio kwa wageni wanapotembelea msitu huu ’’,anasema.

Meneja huyo wa TFS anasema  Hifadhi ya Mwambesi pia ina wanyama wa mtoni kama mamba na viboko ambapo wakati wa masika wanakuwa wengi  na kuvutia wageni wanaobahatika kutembelea msitu huo.

Anasema mtalii akiwa katika msitu wa Mwambesi anaweza kufanya utalii wa kuteleza kwenye mitumbwi katika Mto Ruvuma.

Deborah Mwakanosya ni Meneja wa Msitu wa Hifadhi ya Taifa wa Mazingira Asilia Mwambesi anasema Mwambesi ni msitu wa asili wa pili kwa ukubwa kwa Tanzania ukiongozwa na msitu wa Kilombero mkoani Morogoro.

Anasema msitu huo ambao umezungukwa na Mto Ruvuma, umesheheni baianowai mbalimbali za mimea adimu duniani ikiwemo miti aina ya mipozipozi ambayo ina tabia ya kudondosha maji,miti hiyo inapatikana sehemu chache duniani ukiwemo msitu wa Mwambesi.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.